ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, June 18, 2023

TANZANIA YAZINDUA SIKU YA MSIMBOMILIA 'QR-CODE', WAFANYABIASHARA WAOMBA ENEO LA VIWANDA VIDOGO


Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitaifa wa siku ya GS1 Tanzania (National Barcode day) kwa Wanaviwanda watumiaji wa Msimbomilia (Barcodes), QR-Code na Traceability System katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam Juni 17, 2023.

TANZANIA ni moja kati ya nchi 21 barani Afrika ambazo ni mwanachama katika Shirika la GS1 GLOBAL na zimepatiwa leseni yake.

Wanachama wengine ambao wamepewa leseni hiyo ni Algeria, Misri, Ivory Coast, Kenya, Libya, Mauritius, Morocco, Nigeria, Senegal na Afrika Kusini.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima wakati uzinduzi wa kitaifa wa GS1 Tanzania National Barcode day kwa Wanaviwanda watumiaji wa Msimbomilia (Barcodes), QR-Code na Traceability System katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam Juni 17, 2023. Amesema kutokana na changamoto za kukosa Msimbomilia serikali ina nia thabiti ya kusaidia jumuiya ya wafanyabiashara na sekta binafsi kwa kusimamia na kushiriki katika mchakato wa kuanzishwa kwa taasisi itakayosimamia kisheria utoaji wa huduma za Msimbomilia na Ufuatiliki katika bidhaa zinazozalishwa nchini na nje ya nchi.

Amesema kuwa GS1 Tanzania inatoa alama za utambuzi wa bidhaa za wajasiriamali wadogo wakati na wakubwa ili kusaidia kutafuta wateja kutoka nchi mwanachama na kupanua wigo kujiongezea wateja.

Aidha ametoa wito wito kwa Uongozi na Menejimenti ya GS1 Tanzania kuwa na mikakati ya kuzifikia nchi ambazo zinaizunguka Tanzania na kuhakikisha wanatumia Msimbomilia (Barcodes) za Tanzania ili kuongeza pato na kuitangaza nchi.

“Taasisi za GS1 popote pale duniani pamoja na kutoa huduma za viwango vya kimataifa (Global Standards) katika utambuzi wa bidhaa, pia hutakiwa kusimamia na kuratibu mfumo wa wake, na kushauri sekta za biashara na viwanda katika matumizi yake, kutoa ushirikiano, maoni, ushauri kwa vyama vya biashara, idara za Serikali, makundi ya walaji wa bidhaa, vyama vya kitaalamu na mafunzo kwa wadau wa mfumo huu ukiwamo mfumo wa ufuatiliki wa bidhaa.” Amesema Dkt. Doroth

Akizungumzia kuhusiana na masoko ya nchi za Ulaya na Amerika, Amesema kua suala viwango vya bidhaa ni nyeti kwani hugusa afya ya walaji kutokana na matumizi ya madawa katika kilimo na mifugo ambayo huweza kuathiri afya ya walaji. Suala hilo linatakiwa kutapewa umuhimu mkubwa na taasisi zote zinazosimamia ubora, usalama na viwango vya bidhaa nchini.

Kwa upande wa Afisa Mtendaji Mkuu wa Gs1 Tanzania, Fatuma Kange ameiomba serikali kuwatafutia eneo la Hekari 10 kwaajili y wajasirimali kwaajili ya kutengeneza viwanda vidogo.

Amesema kuwa wajasiliamali hao wanakabiliwa na changamoto ya kukosa maeneo ya kuzalishia bidhaa zao na badala yake wanatumia maeneo yasiyo rasmi katika kutengeneza bidhaa.

Shirika la GS1 GLOBAL lina hati miliki ya huduma mbalimbali ikiwamo ya Barcodes, hutoa leseni kwa taasisi moja kila nchi ili kuendelea kutoa huduma hizo kwa nchi husika. ikumbukwe, si kila nchi Duniani inabahatika kupata tunu hii ya kupewa leseni na GS1 GLOBAL.

No comments: