ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, June 17, 2023

SERIKALI NA CCM KUBORESHA MIUNDOMBINU YA MICHEZO NCHINI



Na Eleuteri Mangi, WUSM, Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amekutana na kufanya kikao cha pamoja na ujumbe kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) ambapo wamejadili namna bora ya kuboresha miundombinu ya michezo nchini.

Kikao hicho kimefanyika Juni 16, 2023 jijini Dodoma ambapo timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo wakiongozwa na Katibu Mkuu wake Bw. Saidi Yakubu na ujumbe wa CCM ukiongozwa na Bw. Mussa Matoroka MNEC na Katibu wa CCM mkoa wa Arusha.

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili kuhusu uendeshaji na usimamizi wa viwanja vya michezo vinavyomilikiwa na kusimamiwa na Serikali pamoja na CCM ambavyo vinatumika katika michezo mbalimbali nchini ikiwemo Ligi Kuu ya NBC.

Kikao hicho kimehudhuriwa wajumbe nane kutoka CCM akiwemo Mhasibu Mkuu wa CCM Taifa Bw. Thobias Abwalo huku ujumbe wa Wizara yenye dhamana na michezo ikiwa na wajumbe saba akiwemo Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo nchini Bw. Ally Mayayi.

No comments: