ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, June 17, 2023

RAIS DKT.SAMIA APOKEA GAWIO LA SERIKALI SH.BIL,45.5 KUTOKA BENKI YA NMB KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 25 YA MAFANIKIO YA BENKI HIYO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea mfano wa Hundi ya Shilingi Bilioni 45.5 (Gawio la Serikali) kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Bi. Ruth Zaipuna kwenye maadhimisho ya miaka 25 ya Benki ya NMB yaliyofanyika Mlimani City Jijini Dar es Salaam tarehe 17 Juni, 2023. Wengine katika picha ni Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NMB Dkt. Edwin Mhede pamoja na Msajili wa Hazina Nehemia Mchechu wakishuhudia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na Wafanyakazi wa Benki ya NMB kabla ya kupokea Gawio la Serikali Shilingi Bilioni 45.5 kutoka Benki hiyo katika maadhimisho ya miaka 25 ya Mafanikio ya Benki Mlimani City Jijini Dar es Salaam tarehe 17 Juni, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akibonyeza kitufe kuashiria kufunga maadhimisho ya miaka 25 ya Mafanikio ya Benki ya NMB katika hafla iliyofanyika Mlimani City Jijini Dar es Salaam tarehe 17 Juni, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Bi. Ruth Zaipuna wakati akielezea Mafanikio ya Benki hiyo tangu kuanzishwa kwake katika hafla iliyofanyika Mlimani City Jijini Dar es Salaam tarehe 17 Juni, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipiga makofi mara baada ya kufunga maadhimisho ya miaka 25 ya Mafanikio ya Benki ya NMB katika hafla iliyofanyika Mlimani City Jijini Dar es Salaam tarehe 17 Juni, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Benki ya NMB wanaohudumu tangu kuanzishwa kwake mara baada ya kufunga maadhimisho ya miaka 25 ya Mafanikio ya Benki hiyo Mlimani City Jijini Dar es Salaam tarehe 17 Juni, 2023.
Viongozi mbalimbali pamoja na Wafanyakazi wa NMB wakiwa kwenye maadhimisho ya miaka 25 ya Mafanikio ya Benki hiyo Mlimani City Jijini Dar es Salaam tarehe 17 Juni, 2023.

No comments: