Wananchi mbalimbali waliojitokeza kuadhimisha siku ya wachangiaji damu Duniani wakiwa katika zoezi la uchangiaji damu ikiwa ni miongoni mwa shughuli za maadhimisho hayo huko Uwanja wa Magirisi Wilaya ya Magharibi B Mika wa Mjini Magharibi.
Wananchi mbalimbali waliojitokeza kuadhimisha siku ya wachangiaji damu Duniani wakiwa katika zoezi la uchangiaji damu ikiwa ni miongoni mwa shughuli za maadhimisho hayo huko Uwanja wa Magirisi Wilaya ya Magharibi B Mika wa Mjini Magharibi
Wananchi mbalimbali waliojitokeza kuadhimisha siku ya wachangiaji damu Duniani wakiwa katika zoezi la uchangiaji damu ikiwa ni miongoni mwa shughuli za maadhimisho hayo huko Uwanja wa Magirisi Wilaya ya Magharibi B Mika wa Mjini Magharibi
Wananchi mbalimbali waliojitokeza kuadhimisha siku ya wachangiaji damu Duniani wakiwa katika zoezi la uchangiaji damu ikiwa ni miongoni mwa shughuli za maadhimisho hayo huko Uwanja wa Magirisi Wilaya ya Magharibi B Mika wa Mjini Magharibi
Waziri wa Nchi (AR) Tawala za Mikoa Serikali za Mitaaa na Idara maalum za SMZ Masoud Ali Mohammed akipata maelezo kuhusiana na zoezi la uchangiaji damu kutoka kwa Meneja wa kitengo cha damu salama Dkt Masuod Ali masoud wakati alipotaka kuzindua zoezi hilo ikiwa ni maadhimisho ya siku ya uchangiaji damu ambayo kitaifa huadhimishwa kila ifikapo juni 14, hafla iliyofanyika uwanja wa magirisi wilaya ya magharibi B Mkoa wa Mjini Magharibi.
Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Hassan Hafidh Khamis akizunguza machache na kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Nchi (AR) Tawala za Mikoa Serikali za Mitaaa na Idara maalum za SMZ Masoud Ali Mohammed kuzindua zoezi la uchangiaji damu katika maadhimisho ya siku ya wachangiaji damu ambayo kitaifa huadhimishwa kila ifikapo juni 14,hafla iliyofanyika juni 15,2023 huko uwanja wa Magirisi Wilaya ya Magharib B Mkoa wa Mjini Magharibi
Waziri wa Nchi (AR) Tawala za Mikoa Serikali za Mitaaa na Idara maalum za SMZ Massoud Ali Mohammed akizingumza na wachangiaji damu (hawamo pichani) wakati akizundua zoezi la uchangiaji damu katika maadhimisho ya siku ya wachangiaji damu ambayo huadhimishwa kila ifikapo Juni 14,hafla iliyofanyika Juni 15,2023 huko Uwanja wa Magirisi Wilaya ya Magharibi B Mika wa Mjini Magharibi.
Waziri wa Nchi (AR) Tawala za Mikoa Serikali za Mitaaa na Idara maalum za SMZ Masoud Ali Mohammed akikamkabidhi zawadi maalum mchangiaji wa damu kundi adimu ( rhesus-) Juma Kombo Dawa wakati wa maadhimisho ya siku ya uchangiaji Damu Duniani ambayo kitaifa huadhimishwa kila ifikapo juni 14, hafla iliyofanyika uwanja wa magirisi wilaya ya magharibi B Mkoa wa Mjini Magharibi.
Waziri wa Nchi (AR) Tawala za Mikoa Serikali za Mitaaa na Idara maalum za SMZ Masoud Ali Mohammed akimkabidhi zawadi maalum mchangiaji bora wa damu Khamis Pandu Khamis ambae ameshachangia mara 56, wakati wa maadhimisho ya siku ya uchangiaji Damu Duniani ambayo kitaifa huadhimishwa kila ifikapo juni 14, hafla iliyofanyika uwanja wa magirisi wilaya ya magharibi B Mkoa wa Mjini Magharibi
Waziri wa Nchi (AR) Tawala za Mikoa Serikali za Mitaaa na Idara maalum za SMZ Masoud Ali Mohammed akisalimiana na kufurahi pamoja na Vijana wa kikosi cha Jeshi la kujenga Uchumi (JKU) wakati wa hafla ya uchangiaji damu iliyofanyika uwanja wa magirisi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya uchangiaji Damu duniani ambayo Kitaifa huadhimishwa kila ifikapo juni 14,hafla iliyofanyika juni 15,2023 huko uwanja wa Magirisi Wilaya ya Magharib B Mkoa wa Mjini Magharibi
Waziri wa Nchi (AR) Tawala za Mikoa Serikali za Mitaaa na Idara maalum za SMZ Masoud Ali Mohammed akisalimiana na kufurahi pamoja na Vijana wa kikosi cha Jeshi la kujenga Uchumi (JKU) wakati wa hafla ya uchangiaji damu iliyofanyika uwanja wa magirisi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya uchangiaji Damu duniani ambayo Kitaifa huadhimishwa kila ifikapo juni 14,hafla iliyofanyika juni 15,2023 huko uwanja wa Magirisi Wilaya ya Magharib B Mkoa wa Mjini Magharibi.
Na Rahma Khamis Maelezo
Waziri wa nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe, Masoud Ali Mhammed amevitaka Vikosi vya SMZ kuendelea kuchangia damu ili kuokoa maisha ya watu katika jamii.
Akizungumza mara baada ya kuzindua zoezi la uchangiaji damu katika Uwanja wa Magirisi Melinne Wilaya ya Magharib B ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya uchangiaji damu Duniani amesema damu ni muhimu kwa mwanadamu kwani bila ya damu hakuna uhai .
Amesema azma ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuimarisha Sekta ya Afya nchini hivyo uchangiaji wa Damu unaofanywa na Vikosi hivyo utasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuimarisha Afya za Wananachi.
Waziri Masoud amefahamisha kuwa damu ni muhimu katika maisha ya kila siku kutokana na uhitaji wake hasa kwa akina mama na watoto pamoja na wanaopata ajali hivyo ipo haja kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kuchangia damu ili kuokoa uhai wa wengine.
"Unapotoa damu ukampa mwengine umeshaokoa uhai kwani sadaka si tende na mali tu, hata kuchangia damu ni sadaka tosha inayokufanya kuekeza mbele ya Mwenyezimungu na wala hupotezi, tena utapata faida duniani na akhera," alisema Waziri.
Aidha amewashukuru vikosi na wananchi kwa ujumla kwa kuchangia damu na kuwataka kutumia vyakula vya kuongeza damu ili kurejesha damu hiyo na kuweza kutoa katika kipindi chengine.
Hata hivyo amevitaka vikosi hivyo kujilinda na kujiweka imara zaidi kwa ajili ya maslahi ya nchi na Taifa kwa ujumla.
Akisoma risala ya maadhinisho ya siku hiyo Sabra Mahamoud Ali kutoka Kitengo cha Damu Salama amesema kitengo cha damu salama kinaadhimisha siku hiyo kwa kuendeleza kuchangia damu salama ili kupunguza tatizo la upungufu wa damu Nchini.
Amesema Wizara ya Afya Zanzibar kwa kushirikiana na Wizara ya Afya Tanzania pamoja na Chama cha Mstalaba Mwekundu (redcroos) zimeanzisha mpango wa damu salama ili kuokoa maisha ya watu
Aidha amefahamisha kuwa ili uweze kuchangia damu lazima kukidhi vigezo vinavyotakiwa ikiwemo umri wa kuanzia miaka 18 ,uzito wa kilo 50 na wingi wa damu usiopungua 12 pamoja na kutokua na maradhi nyemelezi ikiwemo sukari na presha .
Sabra ameeleza kuwa takwimu zinaonesha kuwa sababu kubwa ya kupoteza maisha kutokana na ukosefu wa damu ni mama wanaojifungua na watoto hivyo ipo haja kwa jamii kuhakikisha kama ana sifa kushiriki katika kutoa damu.
Nae mchangiaji bora wa damu ambaye ameshachangia mara hamsini na sita Hassan Pandu Khamis ameipongeza Wizara kwa kumpatia zawadi na kuitaka jamii kujitokeza kwa wingi kuchangia kwani wahitaji ni wengi .
Maadhimisho ya siku ya uchangiaji wa damu Duniani hufanyika kila ifikapo juni 14 ambapo kaulimbiu ya mwaka huu CHANGIA DAMU ,CHANGIA MAZAO YA DAMU, CHANGIA MARA KWA MARA.
No comments:
Post a Comment