ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, June 17, 2023

WATUMISHI WA MAMBO YA NJE WAFANYA USAFI HOSPITALI YA MKOA WA DODOMA KUADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA


Mkurugenzi wa Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen P. Mbundi (mwenye barakoa) akishiriki zoezi la kufanya usafi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma ikiwa ni sehemu ya sherehe za kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma. Balozi Mbundi alimwakilisha Katibu Mkuu, Balozi Samwel Shelukindo. Mwenye miwani ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Dkt. Paul Mageni. Zoezi hilo limefanyika kwenye Hospitali hiyo tarehe 17 Juni 2023. Kaulimbiu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi mwaka huu ni "Kufanikiwa kwa Eneo Huru la Biashara Barani Afrika kunahitaji usimamizi wa Utumishi wa Umma wenye Mtazamo wa Kikanda".
Balozi Mbundi akiwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Salifius Mligo (kushoto) wakiendelea na zoezi la usafi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma.
Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bw. Kawina Kawina naye akiendelea na zoezi la usafi
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi, Bw. Magabilo Murobi (kushoto) akiwa na Afisa Usafirishaji wa Wizara Bw. Maulid Mkenda wakishiriki zoezi la usafi
Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji, Bw. Athuman Nkungu akiendelea na zoezi la usafi
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiendelea na zoezi la usafi
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiendelea na zoezi la usafi kwa kuchoma takataka
Zoezi la usafi likiendelea
Watumishi wa Wizara wakijituma katika zoezi la usafi
Zoezi la usafi likiendelea
Zoezi la usafi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma likiendelea
Zoezi la usafi likiendelea
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje wakiendelea na zoezi la usafi
Zoezi la Usafi likiendelea
Zoezi la usafi likiendelea
Zoezi la usafi likiendelea
Usafi ukiendelea katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma
Zoezi la usafi likiendelea
Watumishi wa Wizara wakishiriki zoezi la usafi
Usafi ukiendelea katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masahariki wakiwa katika eneo la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kwa zoezi la usafi.
Balozi Mbundi (kushoto) akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu mara baada ya Wizara kukamilisha zoezi la usafi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma Bw. Mageni akitoa neno la shukrani kwa Wizara kwa kutembelea Hospitali hiyo
Picha ya pamoja
....Ushiriki wa Wiki ya Utumishi katika Ofisi Ndogo za Wizara-Dar es Salaam
Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambao wapo katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam nao wakishiriki zoezi la usafi katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma. Zoezi hilo limefanyika tarehe 17 Juni 2023.
Sehemu nyingine ya Watumishi wa Wizara waliopo Dar es Salaam wakiendelea na zoezi la usafi katika Taasisi ya Sratani ya Ocean Road kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma

........Ushiriki wa Wiki ya Utumishi wa Umma katika Ofisi ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Zanzibar

Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambao wapo katika Ofisi ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Zanzibar wakishiriki zoezi la usafi katika Hospitali ya Rahaleo kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma. Zoezi hilo limefanyika tarehe 17 Juni 2023
Usafi ukiendelea katika Hospitali ya Rahaleo Zanzibar kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki itaendelea kuratibu upatikanaji wa madaktari bingwa, vifaa tiba na misaada mingine kutoka kwa wahisani kwa ajili ya kuboresha sekta ya Afya nchini.

 

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 17 Juni 2023 na Mkurugenzi wa Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen P. Mbundi wakati wa zoezi la watumishi wa Wizara hiyo kufanya usafi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma ikiwa ni sehemu ya sherehe za kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma.

 

Balozi Mbundi ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu, Balozi Samwel Shelukindo, alisema kuwa Wizara kwa nafasi yake inaendelea na mkakati wa kutangaza utalii tiba hasa kwa nchi jirani, na mafanikio yamenza kuonekana kutokana na sekta ya afya nchini kuimarika na kuwa na uwezo wa kutoa huduma za kibingwa kwa gharama nafuu ukilinganisha na maeneo mengine duniani.

 

Aliendelea kueleza kuwa watumishi wa Wizara ni sehemu ya jamii ya Watanzania na uamuzi wa kufanya usafi katika hospitali hiyo ni moja ya jukumu lao la kuhudumia jamii, kwa sababu usafi ni tiba ya magojwa.

 

Kwa upande wake, Daktari Bingwa wa Magonjwa Hatarishi, Dkt. Paul Julius Mageni ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo ameishukuru Wizara kwa uamuzi wake huo wa kizalendo. Alisema kitendo kilichofanywa na watumishi wa Wizara ni ibada kubwa na kina lenga kuzuia maambukizi ya magonjwa. “Njia nzuri na rahisi ya kutibu ugonjwa ni kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo na usafi ni moja ya njia za kuzuia magonjwa kusambaa”, Dkt. Mageni alisema.

 

Wizara inaendelea kuadimisha Wiki ya Utumishi wa Umma kwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujadili na kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazowakabili watumishi ili kuchagiza ari na motisha kwa watumishi kufanya kazi kwa juhudi na maarifa.

























No comments: