Advertisements

Monday, July 10, 2023

MHE. BALOZI, DKT. ELSIE KANZA AONGOZA SIKU YA MAADHIMISHO YA LUGHA YA KISWAHILI DUNIANI, WSHINGTON, DC

Bendera zikiwakilisha mataifa ya Afrika ndani ya jengo la Ubalozi wa African Union Washington, DC, ambapo Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani uliadhimisha Siku ya Kiswahili Duniani, Ijumaa July 7, 2023 na Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Dkt. Elsie Kanza (hayuopo pichani ) aliongoza maadhimisho hayo. yaliyohudhuriwa na wadau mbalimbali wa lugha ya Kiswahili wakiwemo Waheshimiwa Mbalozi waalikwa pamoja na mwenyeji wao Balozi wa African Union nchini Marekani Mhe. Hilda Suka Mafudze. Picha na Vijimambo Blog
Wa tatu toka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Dkt. Elsie Kanza akiwa katika picha ya pamoja na wageni wake Mabalozi waalikwa, wa Kwanza kushoto ni Balozi wa Eswatini Mhe. Kennedy Fitzgerald Groening, wa pili ni Balozi wa Ukraine Mhe. Oksana Markarova na wa mwisho kulia ni balozi wa Kenya Mhe. Lazarus O. Amayo
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Elsie Kanza akiongoza maadhimisho ya siku ya lugha ya Kiswahili Duniani yaliyofanyika siku ya Ijumaa July 7, 2023 katika jengo la Ubalozi la African Union Washington, DC.
kulia ni Balozi wa African Union nchini Marekani Mhe, Hilda Suka Mafudze  akitoa hotuba ya ufunguzi siku ya maadhimisho ya lugha ya Kiswahili Duniani yaliyofanyika katika jengo la Ubalozi la African Union Washington, DC. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Dkt Elsie Kanza akifuatilia hotuba hiyo. 
Watatu toka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Dkt Elsie Kanza akiwa na wageni wake waheshimiwa Mabalozi walioalikwa kuhudhuria maadhimisho ya siku ya lugha ya Kiswahili Duniani yaliyofanyika siku ya Ijumaa July 7, 2023. Washington, DC.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Dkt Elsie Kanza akiwa na wageni wake waheshimiwa Mabalozi walioalikwa kuhudhuria maadhimisho ya siku ya lugha ya Kiswahili Duniani yaliyofanyika siku ya Ijuamaa July 7, 2023.
Wadau wa lugha ya kiswahili wakifuatilia maadhimisho hayo yaliyofanyika siku ya Ijumaa July 7, 2023 katika jengo la Ubalozi la African Union, Washington, DC nchini Marekani.

Jopo la wadau wa Kiswahili wakijiandaa kuelezea jinsi wanavyoipambania lugha ya kiswahili nchini Marekani kupitia Vyuo Vikuu, Radio , mashuleni zikiwemo taasisi mbalimbali nchini Marekani.
Dkt. Marko J. Mwaipopo kutoka chuo kikuu cha Michigan akielezea uzoefu wa ufundishaji wa lugha ya Kiswahili katika vyuo na taasisi nchini Marekani,
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi.
Dkt. Mwamoyo Hamza kutoka sauti ya Amerika (VOA) akielezea nafasi ya Kiswahili katika tasnia ya habari nchini Marekani.
Bi. Jerusha Weaver MPH,CHES kutoka chuo kikuu cha North Carolina mji wa Chapel Hill akielezea nafasi ya kiswahili katika Diplomasia ya utamaduni nchini Marekani..
Rhonda Pierce mwakilishi wa Tanzania katika taasisi ya Sister City International (SCI) akielezea nafasi ya kiswahili katika kuimarisha mahusiano ya miji dada ya Arusha, Tanzania na Durham, North Carolina nchini Marekani.
Bi.Jasmine Rubama Mkufunzi wa Kiswahili (foreign Servive Institute) akielezea mchango wa Diaspora katika kukuza lugha ya kiswahili nchini Marekani.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Dkt Elsie Kanza akitoa hotuba ya kufunga maadhimisho ya siku ya lugha ya Kiswahili Duniani na kusisitiza kwamba ataendelea kuitangaza na kuipigania lugha hiyo na kuhakikisha inafika mbali nchini Marekani na kimataifa.
Mshereheshaji Tuma Kaisi akiwajulisha jambo wahudhuriaji kwenye maadhimisho hayo.
Juu na chini ni picha za pamoja Waheshimiwa Mabalozi na wadau wa Kiswahili siku ya maadhimisho hayo Ijumaa July 7, 2023, Washington, DC, nchini Marekani.
Juu na chini ni picha mbalimbali Waheshimiwa Mabalozi na wageni waalikwa waliohudhuria maadhimisho hayo ya siku ya Ijumaa July 7, 2023, Washington, DC, nchini Marekani.













1 comment:

Anonymous said...

Muvina nimekuona bwana!
Ulipata fursa ya kuunguruma kdg??? 🤣🤣🤣🤣🤣
Nimefurahi sana kukuona ndani sutttiiiiii👍👍👍👍👍👍