ANGALIA LIVE NEWS

Friday, July 14, 2023

RAIS SAMIA ATOA ARDHI YA HEKARI TANO KWA AJILI YA UJENZI WA OFISI YA UMOJA WA KUDHIBITI MASWALA YA NISHATI AFRIKA MASHARIKI .

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mkurugenzi Mkuu wa EWURA ,Dk James Andilile akizungumza katika kikao hicho jijini Arusha

Julieth Laizer,Arusha.

Arusha .Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania , Samia Suluhu Hassan ametoa ardhi ya hekari tano kwa ajili ya kujenga ofisi za kudumu ya umoja wa kudhibiti maswala ya nishati Afrika mashariki(EREA )kitakachojengwa mkoani Arusha hivi karibuni.

Hayo yamesemwa jijini Arusha na
Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji Tanzania (EWURA ), Dk James Andilile wakati akizungumza katika kikao cha mamlaka ya udhibiti wa nishati kutoka nchi tano za Afrika Mashariki ambazo ni
Uganda ,Rwanda ,Burundi , Kenya na Tanzania.

Dk Andilile amesema kuwa, kituo kitajengwa hapa Arusha na tayari hati zimepatikana na sasa hivi wanaangalia namna ya kuanza utekelezaji haraka ili kuwa na ofisi ya kudumu hapa.

“Tunamshukuru sana Rais Samia kwa kutoa ardhi hiyo ambayo itawezesha kujengwa kwa ofisi pamoja na chuo ambacho kitatoa mafunzo kwa wadhibiti wa umoja huo wa Afrika mashariki.”amesema Dk Andilile.

Amesema kuwa ,uwepo wa chuo hicho nchi yetu itanufaika kwani kuna watu watakuja kupata mafunzo hapa na kuna kipato kitaingia kwani watu watapata mafunzo katika chuo hicho na kuwezeshwa uwepo wa ajira kwa wananchi wetu .

Aidha ameongeza kuwa,lengo la kikao hicho ni kufanya tathmini ya mambo na kubadilishana mawazo na kufanya mipango kwa ajili ya mwaka wa fedha unaokuja 2023 /24 kuhusiana na shughuli za kiutendaji .

Amesema dhumuni la kuwa na chombo hicho ni kuweka uwiano wa maswala ya udhibiti kisheria kikanuni wa kikanda ili kuchochea uwekezaji katika sekta za nishati ili kuimarisha ustawi wa jamii.

“Umoja wa chombo hicho cha Erea umehusisha nchi tano kutoka ukanda wa jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ni , Uganda ,Rwanda ,Burundi , Kenya na Tanzania na huwa tunakutana mara mbili kwa mwaka kwa ajili ya kujadili maswala mbalimbali .”amesema

.Aidha amesema kuwa,kwa mwaka huu mpaka leo Tanzania ndo ilikuwa ni Mwenyekiti wa chombo hicho cha Erea na katika kipindi hicho ambacho Tanzania ilikuwa Mwenyekiti wameweza kufanikiwa kukamilisha swala la usajili wa chombo cha Erea na kitaanza kutekeleza majukumu yake kwa kujibu wa sheria.

Naye Mkuu wa mkoa wa Arusha ,John Mongela akizungumza kwenye kikao hicho amepongeza juhudi mbalimbali zinazofanywa na mamlaka hiyo katika kuhakikisha malengo mbalimbali yanafikiwa kwa wakati na bila kuwepo kwa changamoto zozote.

“Tunamshukuru sana Rais Samia kwa kutoa eneo hilo kwani kwetu sisi mkoa wa Arusha kuwepo kwa ofisi hizo hapa kutasaidia sana mkoa wa Arusha kuendelea kukua na kuonekana kuwa kivutio sambamba na kuongeza wimbi la ajira na kukua kwa uchumi na pato la Taifa kwa ujumla.”amesema Mongela

No comments: