Friday, January 26, 2024

WAZIRI WA SMZ ATANGAZA KUJIUZULU, NI SIMAI MOHAMMED SAID



Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Mhe. Simai Mohamed Said, ametangaza kujiuzulu wadhifa wake kupitia ukanda wa video uliosambaa kwenye mitandao ya kijamii, usiku wa kuamkia leo Ijumaa Januari 26, 2024.

“Usiku huu tarehe 25 mwaka 2024, nimeandika barua rasmi kwenda kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ya kujiuzulu nafasi yangu nikiwa Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale kuanziaq leo.” Amesema katika ukanda huo wa video na kuendelea kusema..

Nimefikia uamuzi huu ambao hapa kwetu si rahisi katika utamaduni wetu, kutokana na imani yangu kwamba jukumu namba moja la wasaidizi wa Mheshimiwa Rais wakiwemo Mawaziri ni kumsaidia kutekeleza Ilani ya Chama, na inapotokea mazingira yasiyo rafiki katika kutekeleza jukumu hilo muhimu kwa ustawi wa wananchi, ni vyema kutafuta jawabu kwa haraka ili kazi ya kuwaletea wananchi maendeleo iweze kuendelea, na hata ikibidi kukaa pembeni. Mimi nimefikia uamuzi huo mgumu wa kukaa pembeni.” amesema

No comments: