Thursday, February 22, 2024

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU YAWAKUTANISHA MAWAZIRI, WATENDAJI WA WIZARA NA WAANDISHI WA HABARI


Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Zuhura Yunus akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 22 Februari, 2024.
Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe amesema Mvua za El Nino zimechangia uhaba wa Sukari nchini na Serikali inafanya juhudi ya kukabiliana na uhaba huo kwa kutoa ruhusa ya waagizaji wapya.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji), Prof. Kitila Mkumbo akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Vyombo mbalimbali waliohudhuria mkutano ulioandaliwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jijini Dar es Salaam, tarehe 22 Februari 2024.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba amesema kauli ya Waziri wa Nishati kuhusu kiasi cha uzalishaji wa umeme pamoja na za Mkuu wa Mkoa wa Dar kuhusu uchakavu wa miundombinu zote ni sahihi.
Prof. Kenneth Besegi Mkurugenzi Bodi ya Sukari akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Vyombo mbalimbali waliohudhuria mkutano ulioandaliwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 22 Februari, 2024.
Balozi Shaibu Said Musa - Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akizungumza na Wahariri wa Vyombo mbalimbali waliohudhuria mkutano ulioandaliwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 22 Februari, 2024.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji), Prof. Kitila Mkumbo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Mramba wakizungumza wakati wa mkutano wa Wahariri, Ikulu Dar es Salaam tarehe 22 Februari, 2024
Balozi Shaibu Said Musa - Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Bw. Gilead Teri wakati mkutano ulioandaliwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 22 Februari, 2024.
Baadhi ya Wahariri na Waandishi kutoka Vyombo mbalimbali vya Habari wakiwa kwenye mkutano ulioandaliwa na Kurugenzi Ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jijini Dar es Salaam, tarehe 22 Februari, 2024.
Baadhi ya Wahariri na Waandishi kutoka Vyombo mbalimbali vya Habari wakiwa kwenye mkutano ulioandaliwa na Kurugenzi Ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jijini Dar es Salaam, tarehe 22 Februari, 2024.

No comments: