ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, February 24, 2024

RAIS DKT. MWINYI AWATEMBELEA WAZEE MBALIMBALI KWA AJILI YA KUWAJULIA HALI ZAO LEO


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kumjulia hali yake Msanii Maarufu wa Zanzibar Bi.Mwapombe Hiyari, alipofika nyumbani kwake Chuini Wilaya ya Magharibi “A” Unguja leo 23-2-2024, ikiwa ni utaratibu wake kuwajulia hali Wazee mbalimbali Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Familia ya Mzee Daudi Suleiman Ali, alipofika nyumbani kwake Fuoni Wilaya ya Magharibi “B” Unguja kwa ajili ya kumsalimia na kumjulia hali yake leo 23-2-2024.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika mazungumzo na Mzee Ramadhan Nzori , aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Jangombe Zanzibar, alipofika nyumbani kwake Jangombe Wilaya ya Mjini Unguja kwa ajili ya mazungumzo na kumjulia hali yake leo 23-2-2024.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuwasalimia Watoto wa Mtaa wa Jangombe Wilaya ya Mjini Unguja leo 23-2-2024, baada ya kumaliza kumzungumza na Mzee Ramadhan Nzori.(Picha na Ikulu)

No comments: