Friday, February 9, 2024

RAIS WA IPU, DKT. TULIA ACKSON AFUNGUA MKUTANO WA KIBUNGE WA UMOJA WA MABUNGE DUNIANI HUKO NEW YORK

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson kwa kushirikiana na Mhe. Dennis Francis, Rais wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UNGA) Februari 8, 2024, wamefungua Mkutano wa Kibunge wa Umoja wa Mabunge Duniani katika Umoja wa Mataifa (2024 Parliamentary Hearing at the United Nations).
Mkutano huu unaofanyika katika Ukumbi wa Kamisheni ya Uchumi na Maendeleo ya Jamii, Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York nchini Marekani, unahudhuriwa na Mabunge ya nchi 180 Duniani na mwaka huu unaangazia mada kuu ya “Amani na Usalama wa Kesho: Nia nzuri ya kuleta matokeo ya pamoja.”

No comments: