ANGALIA LIVE NEWS

Friday, March 1, 2024

HAKUNA MTU ATAKAYEKOSA MATIBABU, MKATABA BAINA YA NHIF NA APHFAT HAUJAVUNJWA - Dkt. SAGWARE


Mwenyekiti wa Kamati ya kupitia kitita cha mafao cha NHIF 2023 Dkt. Baghayo Saqware akizungumza na waandishi wa habari Februari 29, 2024 katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
 
Mwenyekiti wa Kamati ya kupitia kitita cha mafao cha NHIF 2023 Dkt. Baghayo Saqware akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 29,2024 katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam

MWENYEKITI wa Kamati ya kupitia kitita cha mafao cha NHIF 2023 Dkt. Baghayo Saqware amesema maamuzi ya ujio wa Kitita hicho ni matokeo ya makubaliano ya pande zote ambazo ni watoa huduma binafsi za Afya na BAKWATA kwa maslahi ya serikali na sekta binafsi.

Akizungumza leo Februari 29,2024 Jijini Dar es Salaam, Dkt Saqware amesema hakuna atakayekosa huduma ya matibabu kwa kuwa mkataba baina ya mfuko na watoa huduma za afya wa sekta binafsi (APHTA) haujavunjwa.

“Kamati ilikuwa huru kumsikiliza kila mtu, tulikubaliana kwa pamoja na tuliamua kitita kianze kutumika kwa faida ya nchi na taasisi zetu.

“Kwahiyo tunapenda kutoa msimamo wa kitaalam kwamba Wizara kupitia NHIF iendelee na utekelezaji wa kitita cha mafao kilichoboreshwa cha NHIF cha mwaka 2023 kama ilivyoshauriwa na kamati,” amesema Dk Saqware.

Aidha amesema kuwa mapendekezo ya kamati ya wataalam ni pamoja na kuanza kutumika kwa kitita cha mafao cha mwaka 2023 pamoja na maboresho yaliyopendekezwa na kamati katika sehemu ya ada ya ushauri na kumuona daktari, huduma za dawa, upasuaji na vipimo.

Sambamba na hilo amesema Kitita kinachotumika hivi sasa kilifanyiwa maboresho kwa mara ya mwisho mwaka 2016 hivyo Mfuko umelazimika kufanya mapitio katika Kitita hicho ili kwenda sambamba na mahitaji yaliyopo na hali halisi ya utoaji wa huduma za afya nchini.

No comments: