Advertisements

Tuesday, April 16, 2024

DKT. KIKWETE ATEMBELEA CHUO CHA UONGOZI CHA JULIUS NYERERE KILICHOPO NDANI YA CHUO KIKUU CHJA MAKERERE JIJINI KAMPALA, UGANDA



Rais Mstaafu Dkt. Kikwete akiwa na Mkurugenzi wa Kituo cha Uongozi cha Julius Nyerere, Dkt. Nansozi Muwanga alipotembelea Kituo hicho kilichopo ndani ya Chuo Kikuu cha Makerere, Kampala, Uganda, jana Jumatatu.

Kituo hicho, kinachotoa mafunzo ya uongozi na kuandaa vijana kuwa viongozi bora, kinaratibiwa na chuo Kikuu cha hicho kikongwe Afrika Mashariki.

Dkt Kikwete alitembelea chuoni hapo alipoalikwa kama mgeni rasmi katika mkutano mkuu wa kwanza wa marais na viongozi wa sasa na wa zamani wa serikali za wanafunzi wa vyuo vikuu vya Uganda ambapo alialikwa kama mgeni rasmi. Mkutano huo, uliojadili umuhimu na nafasi ya viongozi waliopo madarakani kuandaa viongozi wanaochipukia, ulihudhuriwa na zaidi ya marais na viongozi wa sasa na waliowahi kuwa viongozi wa serikali za wanafunzi wa vyuo vikuu vya nchini Uganda zaidi ya 1,000.

No comments: