Advertisements

Wednesday, April 10, 2024

RAIS WA ZANZIBAR AHUTUBIA BARAZA LA EID FITRY UKUMBI WA CHUO CHA POLISI ZIWANI ZANZIBAR




RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akilihutubia Baraza la Eid Fitry katika ukumbi wa Polisi Ziwani Wilaya Mjini Unguja leo 10-4-2024.(Picha na Ikulu)


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akipokea Salamu ya Heshima katika Sherehe za Baraza la Eid Fitry, katika viwanja vya Chuo cha Polisi Ziwani Wilaya ya Mjini Unguja leo 10-4-2024.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Viongozi wa meza kuu na Wananchi katika kuitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi (kulia kwa Rais) baada ya kumalizika kwa Baraza la Eid Fitry lililofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Polisi Ziwani Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar leo 10-4-2024.
(Picha na Ikulu)

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi amewashukuru Masheikh na Waalimu kwa kazi kubwa ya kuendesha madarasa ya mawaidha katika Misikiti mbalimbali na Mihadhara kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Rais Dk. Mwinyi amewashukuru wafanyabiashara waliotikia wito wa Serikali wa kutopandisha bei za bidhaa ili kuwezesha wananchi kununua bidhaa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani .


Rais Dk.Mwinyi amesema hayo katika Baraza la Eid ukumbi wa Ziwani Chuo cha Polisi, Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 10 Aprili 2024.


Aidha Rais Dk.Mwinyi amewahimiza waumini wa Dini ya Kiislamu kuyaendeleza mafunzo waliyopata kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kudumu kufanya mambo ya heri na kuacha kutenda maovu katika maisha ya kila siku.
Halikadhalika Rais Dk.Mwinyi amesisitiza taasisi za ZAWA, ZECO na Wizara ya Ujenzi kufanya kazi kwa ukaribu na wakandarasi wanaojenga barabara ili kukabiliana na uharibifu wa miundombinu ya maji na umeme na huduma nyingine.


Rais Dk.Mwinyi ameliagiza Jeshi la Polisi kuhakikisha wanasimamia hali ya ulinzi na usalama wa barabarani kipindi hiki cha Sikukuu .


Vilevile amewaomba viongozi wa Dini kuendelea kuiombea Dua nchi na viongozi wake pamoja na kuendelea kudumisha amani na utulivu.






No comments: