Tuesday, May 28, 2024

IGP AWAVISHA ASKARI NISHANI YA MUUNGANO NA UTUMISHI WA MUDA MREFU IKIWA PAMOJA NA TABIA NJEMA

IJP Camillus Wambura akiwavisha nishani ya kumbukumbu ya Muungano na utumishi wa muda mrefu ikiwa pamoja na tabia njema maafisa na askari wa vyeo mbalimbali kutoka Mkoa wa Songwe wakiongozwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe SACP Augustino Senga kwa niaba ya Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan walizotunukiwa wakati wa maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Sherehe hizo za uvalishaji wa nishani zimefanyika mkoani Mbeya Mei 27, 2024 na kuhusisha mikoa ya kanda za nyanda za juu kusini ikiwemo Mbeya, Songwe, Rukwa na Njombe.










No comments: