Tuesday, May 28, 2024

WAZIRI MKENDA AFUNGUA WIKI YA MAADHIMISHO YA KITAIFA YA ELIMU, UJUZI NA UBUNIFU, NBAA YAENDELEA KUTOA ELIMU


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda akizungumza wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu, ujuzi na ubunifu mwaka 2024 yenye kauli mbiu isemayo "Elimu, ujuzi na ubunifu kwa uchumi shindani" yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
Meza kuu
   
Baadhi ya wananchi wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda alipokuwa anafungua Maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu, ujuzi na ubunifu mwaka 2024.
Mfanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Sawa Ngendabanka akitoa elimu kuhusu kazi zinazofanywa na Bodi kwa mwananchi waliotembelea Banda la Bodi hiyo wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu kwa Mwaka 2024.
Afisa Uhusiano na Mawasiliano kutoka NBAA, Magreth Kageya akitoa elimu kwa wafanyakazi wa Benki ya NMB walipotembelea Banda la Bodi hiyo wakati wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu kwa Mwaka 2024.
Afisa kutoka Dativa Mgweno akitoa elimu kwa wanafunzi walipotembelea banda la Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu kwa Mwaka 2024.
Mfanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Sawa Ngendabanka akitoa elimu kuhusu namna ya kufanya mitihani ya Bodi kwa mwananchi aliyetembelea Banda la Bodi hiyo wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu kwa Mwaka 2024.
Afisa TEHAMA kutoka NBAA, Hassan Kawambwa akitoa elimu kwa wanafunzi walipotembelea banda la Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu kwa Mwaka 2024.
Afisa TEHAMA kutoka NBAA, Hassan Kawambwa akimuonesha ada za mitihani ya Bodi mmoja wa wananchi aliyetembelea banda la Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu kwa Mwaka 2024.
Mfanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Sawa Ngendabanka akitoa elimu kwa wanafunzi waliotembelea Banda la Bodi hiyo wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu kwa Mwaka 2024.
Maadhimisho yakiendelea 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema Maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu ni sehemu ya mikakati ya serikali katika kuongeza hamasa ya kukuza elimu ujuzi na ubunifu katika kuchangiza maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Mkenda amesema hayo Mei 27, 2024 jijini Tanga wakati akifungua Maadhimisho hayo ambapo amesema matumizi ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu ni nyenzo zinazosaidia kutatua changamoto za kiuchumi na kijamii pamoja na kuchagiza maendeleo ya nchi yetu kwa ujumla.

‘’Serikali inatambua umuhimu na mchango mkubwa wa elimu, ujuzi na ubunifu katika kuchagiza maendeleo ya kiuchumi na kijamii na imepiga hatua kufikia malengo ya Mipango na Mikakati mbalimbali ya Kitaifa, Kikanda na Kimataifa, ikiwemo Dira ya Taifa 2025, Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26, Sera ya Taifa ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023; Ajenda 2063: The Africa We Want; Malengo ya Maendeleo Endelevu-2030, alieleza Waziri Mkenda.

Aidha amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan imefanya mageuzi makubwa katika sekta ya elimu, ikiwemo ujenzi na uboreshaji wa miundombinu, sambamba na kuanza utekelezaji wa Sera ya elimu na mitaala iliyobreshwa pamoja na kuendelea ujuzi na ubunifu.

No comments: