Advertisements

Wednesday, June 19, 2024

MAREKANI YATANGAZA “BINGO” YA DOLA 250,000 KWA MSINDI WA TEKNOLOJIA NCHINI


Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Mhe. Michael Anthony Battle, Sr. (Picha ya Maktaba)

Mshauri wa Diplomasia ya Umma wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania Jeanne Clark leo katika hafla iliyoandaliwa na AidData/REPOA yenye mada kuu isemayo “Wekeza kwa Watu wa Tanzania” ametangaza kuwa Ubalozi wa Marekani kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani wataendesha shindano la wazi kwa sekta binafsi na/au asasi za kiraia watakaowasilisha maandiko ya miradi yatakayosaidia suluhisho za kibunifu za kukuza ushiriki wa raia, kuimarisha jitihada za kukuza uelewa kuhusu dhima, wajibu na utendaji wa vyombo vya habari (media literacy) na utoaji taarifa sahihi na za kuaminika (information integrity) nchini Tanzania.

“Tunawakaribisha wataalamu wa teknolojia na waleta mabadiliko kutoka nchini kote Tanzania kuwasilisha mapendekezo yao na suluhisho kwa hadhira mbalimbali ikiwa ni pamoja na serikali, asasi za kiraia na sekta binafsi. Hadi taasisi zipatazo nane zitachaguliwa kuwasilisha teknolojia zao kwa jopo la majaji. Miongoni mwazo, taasisi tatu zitachaguliwa kuwa washindi wa shindano hili na kupokea ruzuku zenye jumla ya Dola za Kimarekani 250,000. Miradi au suluhisho zitakazoshinda zitatekelezwa kwa manufaa ya Tanzania pekee.” Amesema

No comments: