Mkali wa Singeli Abdallah Ahmed maarufu Dulla Makabila akiwa jukwaani kutumbuiza katika tamasha hilo la burudani kuelekea uzinduzi wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mkoani Kigoma.
Wasanii wa muziki wa Bongo Fleva na Singeli, Sande Mangu almaarufu Linex na Abdallah Ahmed maarufu Dulla Makabila leo Julai 18,2024 wameingiza shangwe kwa wakazi wa Kigoma kwa kutoa burudani kali katika Tamasha la uzinduzi wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Vikundi mbalimbali vilivyokuwa vikishindana katika tamasha hilo, vikitoa burudani.
Katika Tamasha hilo kundi la Waobama waliibuka washindi katika vikundi vya kucheza dansi vilivyokuwa vikishindanishwa na kukabidhiwa zawadi na Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura, Bi. Giviness Aswile.
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) inataraji juzindua Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura Julai 20, 2024 utakaofanyika katika Uwanja wa Kawawa ulipo Ujiji Kigoma na mgeni rasmi akifaraji kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa.
Wasanii hao waliopanda jukwaani kwa nyakati tofauti kutumbuiza katika tamasha hilo maalum kuelekea uzinduzi wa Ubereshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lililokwenda sanjari na utoaji wa Elimu ya Mpiga Kuru kuhusu Uboreshaji wa Daftari.
Alianza kupanda jukwaani Linex ambaye ni mzaliwa wa Kigoma na ambaye alikuwa uwanja wa nyumbani akiimba baadhi ya nyimbo zake maarufu ukiwepo wimbo maalum wa kuhamasisha watu kujitokeza kuboresha taarifa zao na kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Linex anae tamba kwa sasa na kibao chake cha 'Mahama ya Mapenzi' kabla ya kushika jukwaani alitumbuiza kwa wimbo maarufu aliyeyoimba na wasnii wenzake kutoka Kigoma wa 'Leka dutigite' aliyoimba na kundi lao la Kigoma All Stars akiwa na wasanii wenzake kutoka Kigoma ambao ni Abdu Kiba, Baba Levo, Banana Zorro, Chege, Diamond, Linex, Makomando, Mwasiti, Ommy Dimpoz, Queen Darling, Rachel na mwanasiasa maarufu mzaliwa wa Kigoma Zitto Kabwe.
Makabila yeye nae aliimba nyimbo zake kadhaa ikiwepo 'Pita Huku', 'Furahi', 'Hujaulamba', lakini bila kusahau nyimbo za Simba na Yanga ambazo ziliibua shjangwe kubwa jukwaani.
Makabila atatumbuiza tena siku ya Uzinduzi Julai 20,2024 mbele ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa.
Wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Kawawa Kigoma Ujiji walionesha kufurahishwa na burudani hiyo iliyokonga nyoyo zao vilivyo.
Aidha, Mbali na Dulla Makabila na Sande Linex pia vikundi mbalimbali vya burudani kama Warumba Shauri, Smart Boys , Vijana Rumba, Chama Dansa, Mwandiga One, Waobama.
Katika Tamasha hilo kundi la Waobama waliibuka washindi katika vikundi vya kucheza dansi vilivyokuwa vikishindanishwa na kukabidhiwa zawadi na Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura, Bi. Giviness Aswile.
No comments:
Post a Comment