ANGALIA LIVE NEWS

Friday, July 19, 2024

PSPTB YATANGAZA MATOKEO YA MITIHANI YA 28


Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Bw. Godfred Mbanyi akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza matokeo ya mitihani ya 28 ya PSPTB iliyofanyika kuanzia 13 Mei hadi 17 Mei, 2024 katika vituo sita vya mitihani Tanzania bara na Visiwani.
Baadhi ya Menejimenti ya Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) ikifuatilia maelezo ya Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Bw. Godfred Mbanyi alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza matokeo ya mitihani ya 28 ya PSPTB iliyofanyika kuanzia 13 Mei hadi 17 Mei, 2024 katika vituo sita vya mitihani Tanzania bara na Visiwani.

Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imetangaza rasmi matokeo ya mitihani ya 28 ya PSPTB iliyofanyika kuanzia 13 Mei hadi 17 Mei, 2024 katika vituo sita vya mitihani Tanzania bara na Visiwani.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB Godfred Mbanyi amesema jumla ya watahiniwa wapatao 1,280 walisajiliwa ili kufanya mitihani hii ambapo watahiniwa 1,197 (93.5%) walifanya mitihani hii ikiwa ni ongezeko la watahiniwa ukilinganisha na msimu uliopita ulikuwa na watahinwa 977.

Mbanyi amesema kati ya watahiniwa 1,280 jumla ya watahiniwa 551 sawa na 46.0% wamefaulu mitihani yao, watahiniwa 632 sawa na 52.8% watarudia baadhi ya masomo kuanzia somo moja mpaka masomo matatu kutegemeana na masomo idadi ya masomo aliyofeli, na watahiniwa 14 sawa na 1.2% wamefeli masomo yote waliyofanya katika ngazi zao.

Amesema katika masomo 39 waliyopimwa watahiniwa, masomo 24 yalifanywa vizuri, na masomo saba yalifanywa kwa wastani na masomo nane yalikuwa chini ya wastani ambapo kwa ujumla watahiniwa wa kike walifanya vizuri ukilinganisha na watahiniwa wa kiume hii inapelekea ufaulu wa jumla watahiniwa wawili wakike wakiibuka watahiniwa bora katika ngazi za mitihani za Graduate Professional I, na CPSP.
Mbanyi amesisitiza kuwa mikakati ya PSPTB kwa siku za mbele ni kuendelea kuimarisha na kusimamia ubora wa mafunzo yanayotolewa na vituo vya kuwaandaa watahiniwa review centers pamoja na kuimarisha mahusiano ya kitaaluma na Taasisi za elimu ya Juu na Kati ili kuongeza ubora na ufaulu katrika mitihani ya PSPTB.

Pia amesema PSPTB itaendeleaa kuhimiza na kusimamia uanzishwaji na uendeshaji wa mafunzo kwa kutumia fursa ya nyezo za mitandao zilizopo ikiwemo kufanya ziara za kimafunzo vyuoni na katika vito vya mafunzo vilivyosajiliwa na PSPTB ili kuhamasisha usomaji wenye tija kwa ajili ya utendaji mzuri katika mitihani ya PSPTB pamoja na kutembelea vyuo mbalimbali vinavyofundisha taaluma ya Ununuzi, Ugavi, Usafirishaji , kushiriki maonesho mbalimbali yakiwemo ya kitaaluma na kutoa aelimu ya umuhimu wa kufanya mitihani ya PSPTB.

No comments: