Thursday, October 10, 2024

MAKAMU WA RAIS BENKI YA DUNIA ASAFIRI KWA SGR


Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Bi. Victoria Kwakwa (kushoto), akizungumza na Afisa Mwandamizi wa Benki hiyo, Bi. Makiko Watanabe, wakati wakisafiri kwa njia ya Treni ya Kisasa-SGR kuanzia Dar es Salaam hadi Dodoma ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 3 nchini Tanzania kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Benki ya Dunia. Katika ziara hiyo, anatarajia kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), kuhusu ufadhili wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na uwezekano wa Benki hiyo kushiriki katika ufadhili wa vipande vya SGR vilivyosalia.
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Bi. Victoria Kwakwa (kushoto mwenye nguo nyekundu), akiwa na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bw. Nathan Belete, na Maafisa Waandamizi wa Benki hiyo Bw. Nicholas Soikan na Bi. Makiko Watanabe, katika Treni ya Kisasa-SGR wakati wa Safari yao kuanzia Dar es Salaam hadi Dodoma ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 3 nchini Tanzania kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Benki ya Dunia. Katika ziara hiyo, anatarajia kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), kuhusu ufadhili wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na uwezekano wa Benki hiyo kushiriki katika ufadhili wa vipande vya SGR vilivyosalia.
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Bi. Victoria Kwakwa (wa pili kushoto) akiwa na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bw. Nathan Belete (kushoto), wakielekea kupanda Treni ya Kisasa-SGR wakati wa Safari yao kuanzia Dar es Salaam hadi Dodoma ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 3 nchini Tanzania kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Benki ya Dunia. Katika ziara hiyo, anatarajia kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), kuhusu ufadhili wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na uwezekano wa Benki hiyo kushiriki katika ufadhili wa vipande vya SGR vilivyosalia.
Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bw. Nathan Belete (kulia), akizungumza na Afisa Waandamizi wa Benki hiyo Bw. Nicholas Soikan, katika Treni ya Kisasa-SGR wakati wa Safari yao na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Bi. Victoria Kwakwa (Hayupo pichani) kuanzia Dar es Salaam hadi Dodoma ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 3 nchini Tanzania kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Benki ya Dunia. Katika ziara hiyo, anatarajia kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), kuhusu ufadhili wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na uwezekano wa Benki hiyo kushiriki katika ufadhili wa vipande vya SGR vilivyosalia.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dar es Salaam)

Na. Benny Mwaipaja, Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Bi. Victoria Kwakwa, amesafiri kwa njia ya Treni ya Kisasa-SGR kuanzia Dar es Salaam hadi Dodoma ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 3 nchini Tanzania kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Benki ya Dunia. Katika ziara hiyo, anatarajia kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), kuhusu ufadhili wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na uwezekano wa Benki hiyo kushiriki katika ufadhili wa vipande vya SGR vilivyosalia.

Bi Kwakwa alitumia fursa hiyo kuipongeza Tanzania kwa uwekezaji mkubwa wa mradi huo wa SGR ambao amesema utakuwa kichocheo kikubwa cha usafirishaji wa abiria na mizigo na kuchangia ukuaji wa uchumi si tu kwa Tanzania bali kwa nchi zote za Ukanda wa Maziwa Makuu.

Katika safari hiyo Bi. Kwakwa aliambatana na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bw. Nathan Belete, na Maafisa Waandamizi wa Benki hiyo Bw. Nicholas Soikan na Bi. Makiko Watanabe.

No comments: