Thursday, October 10, 2024

TAUHIDA ATOA MSAADA WA SARUJI NA MCHANGA JIMBO LA DIMANI


Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Magharibi Mhe.Tauhida Galos Nyimbo akikabidhi Saruji na Mchanga kwa Viongozi wa Jimbo la Dimani Mkoa wa Mjini Magharibi.

Na Takdir Ali. Maelezo.
Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Magharibi Mhe. Tauhida Galos Nyimbo ameahidi kushirikiana na Viongozi wengine katika kutatua matatizo mbalimbali ya Wananchi.

Akikabidhi Mchanga na Saruji kwa Viongozi wa CCM Jimbo la Dimani Mhe. Tauhida amesema lengo la kutoa msaada huo ni kusaidia kuifanyia matengenezo Ofisi ya Jimbo hilo ili iweze kufanya kazi kwa ufanisi.

Mhe. Tauhida ameahidi kuendelea kushirikiana na Viongozi wa Jimbo hilo katika kuwaletea maendeleo Wananchi na kufikia malengo yaliokusudiwa.

Aidha amewataka kufanya kazi kwa bidii na kuachana na majungu, fitna na uhasama jambo ambalo litapelekea kushindwa kutekeleza mikakati waliojipangia ya kuwaletea maendeleo Wananchi.

Kwa upande wake Katibu wa UWT Wilaya ya Dimani Rehema Haji Makame amesema maendeleo hayo yameweza kupatikana kutokana na mashirikiano yaliopo baina ya Wananchi, Serikali na Chama cha Mapinduzi.

Hata hivyo amewataka kushirikiana katika kudumisha suala la amani na utulivu lililopo nchi ili Viongozi waendelee kuwaletaea maendelao Wananchi.

Nae Mbunge wa Jimbo la Dimani Mhe. amempongeza Mhe. Tauhida kwa juhudi kubwa anazichukuwa katika kuwatumikia UWT, Chama cha Mapinduzi na Wananchi kwa ujumla.

Hivyo ameahidi kushiriikiana na kuwa kutu kimoja ili kuweza kufikia malengo yaliopangwa na Serikali.

No comments: