ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, October 22, 2026

ANDREW CHALE ASHEREKEA BIRTHDAY NA WATOTO WA SHALOM NDANI YA NGORONGORO


Karatu - Ngorongoro.

Mdau wa Utalii  na Mazingira Andrew Chale ametimiza miaka 41 kwa tukio la kipekee ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro akiwa na watoto wa Kituo cha Shalom - Karatu.

Tukio la 'Karibu Nyumbani sherekea na Ngorongoro' limefanyika 21 Oktoba, 2026, limewezeshwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) ambapo Watoto wametembelea Makumbusho ya Olduvai Gorge kujifunza historia ya binadamu na kushuhudia wanyama ndani ya Bonde la Ngorongoro.

"Shukrani kwa NCAA. Nitoe wito kwa Watanzania tutumie vivutio vyetu vya ndani kusherekea siku ya kuzaliwa ama mafanikio." Amesema Chale.

Mbali na ziara ya Utalii Ngorongoro, pia ametoa zawadi katika kituo hicho cha Shalom Orphanage.

Huo ni utaratibu wa kila 21 Oktoba kusherekea siku yake ya kuzaliwa na makundi maalum na wenye uhitaji.












































No comments: