ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, February 16, 2010

Champions League,AC Milan 2 - 3 Man Utd

Wayne Rooney akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kupachika magoli 2  

Manchester United waitesa AC Milan
Manchester United wameimarisha nafasi yao katika michuano ya kuwania kilabu bingwa Ulaya kwa kuishinda AC Milan mabao 3-2.
Ulikuwa ni ushindi wa kwanza wa Man U katika uwanja wa San Siro.
AC Milan walikuwa wa kwanza kuona lango kupitia machachari Ronaldinho mnamo dakika ya tatu tu!
Lakini kabla ya mapumziko Man U walisawazisha wakati mpira uligonga guu la Paul Scholes na kujipinda taratibu hadi wavuni.
Man U walianza kipindi cha pili kwa kishindo huku Rooney akitatiza walinzi wa AC Milan kiasi cha kufunga mabao mawili.
Huku dakika zikiyoyoma, AC Milan walionekana kuongeza kasi na kufunga bao la pili kupitia Clarence Seedof.
Dosari kwa ushindi wa Man U ilitokea pale mchezaji Michael Carrick alipoonyeshwa kadi nyekundu.
Katika matokeo mengine ya michuano hiyo, timu ya Ufaransa ya Lyon iliilaza Real Madrid ya Uhispania bao 1-0.

No comments: