Vituko na simanzi vimetawala nyumbani kwa Mzee Naftal Chacha (60), mkazi wa Ukonga ambaye ni mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), baada ya hausigeli wake, Odillia Mikka (15), kukutwa chumbani kwake akiwanga huku akiwa amekaa ndani ya ungo.
Ilikuwa kama mchezo wa kuigiza katika nyumba hiyo baada ya mtoto wa mwenye nyumba hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Miriam Naftal kumkuta msichana huyo akiwa amechuchumaa ndani ya ungo uliosheheni ndumba kibao pamoja na nguo za ndani za mtoto mkubwa wa kike wa familia hiyo.
Miriam baada ya kuingia katika chumba hicho ghafla alianza kupiga mayowe kumshtua msichana huyo ambapo familia nzima iliyokuwamo ndani ya nyumba hiyo iliingia chumbani huko ili kujionea kinachoendelea.
habari zaidi
Bofya Hapa
No comments:
Post a Comment