ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, February 16, 2010

Makocha wazawa waikacha Taifa Stars


Vicky Kimaro

LICHA ya kutangaziwa vigezo na kupewa ahadi ya kufikiriwa kwanza katika kazi ya ukocha wa Taifa Stars, makocha wazalendo wameiogopa nafasi hiyo.

Wengi wa makocha hao waliiambia Mwananchi katika mahojiano na kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam na mikoani wakieleza kwamba hawawezi kuomba nafasi hiyo kama ilivyo tangazwa na Shiirkisho la Soka Tanzania (TFF).

Makocha hao wengi wao wameonyesha kuwa kauli ya TFF ni sawa na kuwakejeli kwa madai kuwa mfumo mzima wa uongozi ndani ya shirikisho hilo na serikali umeathiriwa na mapenzi kwa vitu vya nje na kuvidharau vile vya ndani.

Wamedai kuwa bora kocha wa Kizungu ndio waendelee kuifundisha Starskwa vile hawataki wachezaji wa timu ya taifa kupata shida.

Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya wanawake, 'Twiga Stars' Seleman Gwaje alisema "Acha mzungu aje tupate maendeleo kwa sababu anapokuwa mzalendo hupewi ushirikiano unaotakiwa, kocha wa kizalendo wachezaji kambi inakuwa hosteli za TFF, lakini mzungu watakaa hotelini tena zile za bei mbaya, hatutaki wachezaji wapate shida,"alisema Gwaje.

"Kocha mzalendo wachezaji hawatapewa chakula kizuri, pesa hakuna, huduma mbovu, lakini mzungu atapewa kila anachokitaka kama Marcio Maximo anavyopewa, Maximo leo akienda kucheza mechi Nairobi (Kenya) watapanda ndege, lakini angekuwa mzawa wanapandishwa basi........

No comments: