ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, February 16, 2010

Marekani kuzalisha kawi ya Nuclear


Rais wa Marekani Barack Obama, ameunga mkono kutengenezwa kwa vinu vya kuzalisha kawi ya nuclear nchini Marekani baada ya miongo mitatu.
Obama amesema Marekani inahitaji kuzalisha kawi safi ya nuclear ili kuweza kukidhi mahitaji yake na vile vile kukabiliana na mabadiliko ya hali ya anga.
Wakati huo huo ameahidi kusimamia mkopo wa dola biloni nane utakaotumika kugharamia ujenzi wa kiwanda cha kwanza lakini sharti kuwepo sheria ya itakayolinda mazingira dhidi ya uharibifu kuambatana na mpango huo.
Uamuzi huo hata hivyo umekosolewa na wanaharakati wa nguvu za nuclear, wa kikundi kijulikanacho kama Beyond Nuclear, ambacho kimesema mpango huo haupaswi kutekelewzwa.

No comments: