ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, March 16, 2010

Nigeria igawanywe pande mbili asema Gaddafi

anali Muammar Gaddafi wa Libya
Kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi amesema Nigeria haina budi kugawanywa na kuwa mataifa mawili kuepuka umwagikaji zaidi wa damu baina ya Waislamu na Wakristo.
Akiwahutubia wanafunzi, amepongeza mfano wa India na Pakistan, ambapo kugawanywa nchi hizo kumeokoa maisha ya watu wengi.
Shirika la Habari la Libya, Jana likimkariri Kanali Gaddafi, akisema "Kuigawanya Nigeria, kutasaidia kukomesha umwagikaji wa damu na uchomaji majengo ya ibada."
Mwanadiplomasia mmoja mwandamizi wa Nigeria hakutilia maanani mapendekeo hayo ya Kanali Gaddafi.
Mamia ya watu wamekufa katika machafuko ya kidini vijijini sehemu mbalimbali za katikati ya Nigeria kwenye mji wa Jos mwaka huu.
Nigeria kwa kiasi kikubwa imegawanyika baina ya Waislamu upande wa kaskazini na Wakristo walio wengi kusini.

No comments: