ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, March 16, 2010

Upasuaji wa Beckham wafanikiwa


  Daktari ambaye anamhudumia Kiungo wa kati wa AC Milan David Beckham amesema kuwa upasuaji huo umefanikiwa.
Lakini daktari huyo , Sakari Orava, amesema jeraha hilo la mshipa wa kisigino linamaanisha Beckham hataweza kucheza kwa muda wa karibu miezi sita .
Nyota huyo aliumia jumapili wakati wa mechi kati ya AC Milan na Chievo. Beckham alikuwa anatumaini kuwa angeweza kuwa mchezaji wa kwanza wa timu ya Uingereza kucheza katika mechi za kombe la dunia mara nne mfululizo.
 

No comments: