ANGALIA LIVE NEWS

Monday, March 1, 2010

Nyota wa kikapu nchini wamfariji Hasheem

 NYOTA wa kikapu nchini, wamesema kuondolewa katika kikosi kinachoshiriki Ligi Kuu ya Kikapu (NBA) cha Memphis Grizzlies ya nchini Marekani kwa nyota wa Tanzania, Hasheem Thabeet, sio tatizo; anachopaswa kufanya ni kuongeza bidii.
Ingawa mashabiki wengi walionyesha kuhuzunishwa na kilichomkuta nyota huyu, baadhi ya wachezaji wa hapa nchini, wamesema hilo sio tatizo na kinachotakiwa kwa nyota huyo kwa sasa ni kutulia na kuonyesha uwezo.
Mmoja wa wachezaji hao Mussa Haroun wa timu ya Vingunguti, alisema kuwa Ligi ya NBA ni ngumu kutokana na kusheheni nyota kutoka kila pembe ya dunia, hivyo wapenzi wasihofu na wala Hasheem hapaswi kukata tamaa.
“Mimi naona hata hivi Hasheem amejitahidi sana kwa sababu ligi ile ni ngumu; inajumuisha nyota wa kikapu kutoka dunia nzima, naamini akifanya mazoezi ya kutosha atarejeshwa,” alisema Haroun

No comments: