ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, March 21, 2010

Pendekezo Kenya Senate wawe wanawake


Kamati ya Bunge ya Kenya inayojadili vipengele vya katiba mpya imependekeza nusu ya wajumbe wa baraza jipya la senate litakalokuwa na uwezo mkubwa wawe wanawake.
Kamati hiyo inayojumuisha vyama vyoye vya kisiasa bungeni ilisema kila mkoa utachagua mwanaume mmoja na mwanamke mmoja katika baraza la Senate, huku nafais nyingine kumi zikitengwa kwa ajili watu kutoka jamii ndogo ndogo.
Kumekuwa na mvutano mkali kuhusu aina ya katiba inayohitajika, ambayo bado inahitaji kuidhinishwa na bunge la Kenya pamoja na Rais, kabla ya kupigiwa kura ya maoni na wananchi ambayo inayotarajiwa kufanyika mwezi Juni mwaka huu.

No comments: