
Kanisa katoliki limeshutumu vikali vyombo vya habari kwa namna vimeripoti visa vya dhulma ya mapenzi dhidi ya watoto wadogo vilivyoendeshwa na baadhi ya makasisi wa kanisa hilo.
Kanisa limetaja hatua hiyo kama njama ya kumchafulia jina Baba Mtakatifu Benedict wa kumi na sita.
Makao makuu ya kanisa hilo yalikuwa yanaashiria habari zilizochapishwa awali kuwa papa huyo, alipokuwa kadinali anayeangazia malalamiko ya dhuluma za kimapenzi, alijaribu kuficha ukweli kuhusu kasisi mmoja aliyeshutumiwa kuwadhulumu zaidi ya watoto mia mbili katika shule moja ya viziwi nchini Marekani.
No comments:
Post a Comment