ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, June 10, 2010

MAMA SALMA ZIARANI MAREKANI

Juu na chini,Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama salma Kikwete na ujumbe wake w akizungumza na uongozi wa Elizabeth Glaser Pediatric Foundation, (EGPAF), ulioongozwa na Bwana Chip Llyons,(kushoto}, wakati Mama Salma aliotembelea Makao Makuu ya shirika hilo nchini Marekani tarehe 86.2010
Juu na chuni,Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na Balozi Nancy Brinker, Mwanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Susan Komen for the cure nchini Marekani. Mazungumzo ya Mama Salma na Balozi Nancy yalifanyika katika ubalozi wa Canada nchini Marekani tarehe 8.6.2010. Baada ya mazungumzo yao Mama Salma alimkabidhi Balozi zawadi ya picha
Juu na chini,Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akisalimiana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii wa Marekani Mheshimiwa Kathleen Sebellius na baadaye kupiga picha ya pamoja katika siku ya pili ya mkutano wa pili wa dunia wa "Women Deliver" unaofanyika jijini Washington DC nchini Marekan
Juu na chini,Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisis ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akisalimiana na baadaye kufanya mazungumzo na Afisa Mtedaji Mkuu wa Millenium Challenge Cooperation,MCC, Bwana Daniel Yohannes. Mazungumzo ya Mama Salma na Afisa Mtendaji huyo yalifanyika katika hoteli ya The Jefferson, huko Washington DC tarehe 8.6.2010
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Mama Shadya Karume,mke wa Rais wa Zanzibar (kulia), na Mke wa Waziri Mkuu wa Waziri Mkuu wa Kenya Mama Ida Odinga na wageni wengine waliohudhuria mkutano wa pili wa "Women Deliver" wakishiriki katika uzinduzi rasmi wa Susan Komen Global Health Foundation uliofanywa na Balozi Nancy Brinker wakati wa chakula cha usiku alichowaandalia wajumbe wa mkutano huo. Sherehe ya uzinduzi huo ilifanyika jijini Washinton nchini Marekani tarehe 8.6.2010
PICHA NA JOHN LUKUWI

No comments: