Fatuma Noah akiwa na vazi la ubunifu
Juliana Varelian akiwa na vazi la ubunifu..
Miss Inter college atamba kunyakua taji la Miss Tanga
Na Andrew Chale
Miss Inter College, Juliana Valelian aliyenyakua taji hilo lililoandaliwa na kampuni ya 5-five Entertainment, mbali ya taji hilo pia alinyakua taji la Miss Lushoto.
Juliana ambaye alinyakua taji hilo la Miss Inter College hivi karibuni na kuwabwaga warembo wenzake 10 kutoka katika vyuo vilivyokuwa ndani ya Wilaya hiyo ya Lushoto, alisema kuwa ameweza kutimiza ndoto yake ya kufika mbali.
“Niliposhinda taji la miss Inter college, niliweka nia ya kufika mbali na kuweza kunyakua taji la Miss Lushoto” alisema Juliana.
Juliana anasema kuwa licha ya kushinda taji hilo la Miss Lushoto na kufanikiwa kuingia katika kinyang’anyilo cha Miss Tanga, amesema amejiandaa vya kutosha katika kambi yao hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa 5-Five Entertainment, Fredo Peter Panyika, alisema kuwa kampuni yake hiyo itaendelea kufanya shughuli za urembo ilikuwainua tasnia hiyo ya Urembo hapa nchini.
caption; Waliokaa watatu; Kutoka kulia ni Happness (kutoka chuo cha IJA) wa katikati aliyekaa ambaye ni mashindi wa kwanza ni Juliana Varelian (IJA), na wa Fatuma Ibrahim Noah (kutoka chuo cha SEKUGO)



1 comment:
hongera sna 5-five entertainment kwa event mliyosababisha karibuni sana pande za kwetu A-TOWN makumira we are waitin 4u guyz(wakali wa burudani tano)
Post a Comment