ANGALIA LIVE NEWS

Monday, July 26, 2010

kutoka mahakama ya kinondoni leo!! Maafisa Afya kizimbani kwa kupokea rushwa

Na Andrew Chale
MAAFISA Afya  Wilaya ya Kinondoni wamepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya kiasi cha shilingi laki moja kutoka kwa muuza duka.
Watuhumiwa hao  walipandishwa kizimbani jana  kusomewa maelezo ya awali ni Ezra Gula (28) na Gelma Chifunda (39) ambao wote ni waajiliwa wa Serikali kitengo cha afisa afya Wilaya ya Kinondoni wakazi wa Mbezi ambapo walikamatwa Julai 21 na Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) baada ya kuwekewa mtego.
Wakisomewa maelezo ya awali na Mwanasheria wa TAKUKURU mkoa wa Kinondoni Ronald Manyiri alidai  kuwa; watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Julai 21 huko Mwananyamala Kinondoni watuhumiwa walikihuka majukumu yao kwa kuomba hongo,  baada ya kufanya ukaguzi wa duka la Simon Shilayo ambapo walipokagua walibaini baadhi ya bidhaa zilikuwa zimekwisha muda wake (expire)
hivyo walimtaka Shilayo awape kiasi cha shilingi laki moja iliwasimchukulie hatua hata hivyo baada ya kukubaliana muuza duka huyo aliweka mitego ya TAKUKURU na kufanikiwa kuwakamata.
Watuhumiwa hao walikana kosa hilo ambapo waliachiwa kwa dhamana ya shilingi laki mbili kila mmoja pamoja na wadhamini wawili wawili ambapo kesi imehairishwa hadi Agosti 16 mwaka huu.

No comments: