
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Sethi Kamuhada (katikati) akimkabidhi zawadi ya kinyago cha saa ya ukutani aliyekuwa Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Marcio Maximo, (kushoto) katika hafla ya kumuaga iliyoandaliwa na Wizara hiyo na kufanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar as Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Tanzania, Leonard Thadeo.
Hapa Maximo akiwa sambamba na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa, (BMT), Kanali mstaafu Idd Kipingu, wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Sethi Kamuhada ambaye haonekani pichani.
Maximo amemaliza muda wake wa kuifundisha timu hiyo baada ya kuinoa kwa kipindi cha miaka mitatu bila kutwaa kombe lolote japo alifanikiwa kuipeleka katika fainali za kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) mwaka 2009.
(Picha na Ahadi Kakore wa Global Publishers

No comments:
Post a Comment