ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, October 26, 2010

TOFAUTI KATI YA MAPENZI YA NDOA NA YA NJE YA NDOA

Sifa za mapenzi ya kweli ni tatu ambazo ni KUJALIANA, KUJITOLEA NA TENDO LA NDOA. Hizi kwa ujumla wake hutumika kwa aina zote mbili za mapenzi, yaani yale ya wanandoa na wapenzi wa kawaida wanaojifurahisha kwa zawadi hiyo ya Mungu.

Kama mtaalamu wa masuala ya mapenzi naweza kusema kwamba, ili watu wawe katika mapenzi sahihi lazima watumikie sifa hizo tatu, yaani kila mmoja awe tayari kujitolea kumsaidia mwenzake kwa kila hali na kwa gharama yoyote.

Kama hilo halitoshi lazima mwenye penzi la kweli awe na sifa ya kumjali mpenzi wake, yaani kumfanya awe wa kwanza na kuwa tayari kupoteza sehemu ya faida yake kwa ajili ya kumridhisha mwenzake katika yale ayapendayo.

Jambo la tatu linaloashiria penzi la kweli lipo kwenye kipengele muhimu kinachoitwa tendo la ndoa. Wapenzi walio ndani ya penzi la kweli lazima watii kiu ya miili yao kwenye suala hili kwa kiwango cha kutoshelezana kabisa.

Ni ukweli ulio wazi kwamba hakuna nyongeza kwenye penzi la kweli endapo hayo matatu niliyotaja yatatimizwa. Lakini ili kuwepo na makundi mawili ya mapenzi niliyoyataja lazima sifa hizo zibadilike mpangilio wake kulingana na kundi la wapenzi.

Wapenzi wanandoa hawawezi kuwa na mambo hayo matatu kwa mpangilio sawa na walio katika uhusiano wa kimapenzi wa kawaida. Tatizo hilo likitokea, uhai wa ndoa huwa mfupi. 

Tumejifunza sifa tatu, lakini hatujaangali mpangilio unaotofautisha penzi la wanandoa na lile la wastarehesha miili, labla ni vema nikaweka wazi suala hili kwa kutenga mfumo huo kama ifuatavyo:

Mpangilio wa sifa za wapenzi wanandoa ni huu KUJALIANA+ KUJITOLEA=TENDO LA NDOA. Kwa wale wa uhusiano wa kimapenzi wa kawaida mfano wanafunzi wao huwa na mpangilio ufuatao. TENDO LA NDOA+KUJALIANA=KUJITOLEA.

Ukiangalia kwa umakini utabaini kuwa sifa zote tatu nilizozitaja zimepatikana kwenye makundi hayo na bila shaka hapa tunazungumzia watu walio katika mapenzi ya kweli si matapeli ambao hukosa sehemu ya sifa hizi.

Kwa kuzingatia mfumo huo, hatutegemei hata kidogo watu walio kwenye ndoa wakaishi kwa mfumo wa walio nje ya ndoa, wakifanya hivyo matatizo na migogoro mingi itaibuka.

Kwa mfano, wapenzi wanafunzi ambao hukutana mara moja kwa wiki au kwa njia za ‘wizi,’ wanapopata nafasi ya kuwa pamoja jambo la kwanza lenye msukomo wa juu huwa ni tendo la ndoa, baada ya hapo huja kwenye kujaliana na baadaye kuamua kujitolea.

Ni vigumu sana kwa mapenzi ya nje ya ndoa kuongozwa na kuelezana matatizo na kujitolea. Vijana wengi hasa wa kiume huona kero kuelezwa matatizo ya familia za wapenzi wao na kuombwa msaada wa vocha na chakula.

Kitu bora kabisa kwenye uhusiano huu wa mapenzi huwa ni kujali zaidi miito ya miili na kuitimizia. “Nimekukumbuka sana mpenzi lini tutakutana?” Wapenzi wengi wa nje huulizana, swali ambalo ni nadra kulipata ndani ya wanandoa.

No comments: