Advertisements

Tuesday, December 7, 2010

John Ndunguru afanya mambo Bongo.

Kijana wa kitanzania aishiye hapa hapa DMV, John Ndunguru, amefanya vitu vyake bongo baada ya kuamua kuinvest nyumbani na kushusha ndege mbili. Kampuni ya John Ndunguru iitwayo Bold Air, imefunguliwa na naibu waziri wa viwanda na biashara, mheshimiwa Lazaro Nyalandu. Mjasilimari John Ndunguru amesema kuwa ameanza na ndege mbili ambazo zitakuwa zikifanya safari zake sehemu mbalimbali nchini. Blog ya vijimambo inampa hongera sana na inawaomba watanzania wengine wafuate mfano wa John. Pichani ni John akiwa na Mheshiwa waziri katika uzinduzi huo wa Bold Air.


(Picha kwa hisani ya michuzi blog)

1 comment:

Anonymous said...

HONGERA..HII NI GREAT NEWS KWA MAENDELEO YA NCHI YETU. JAMANI TUFUATE MFANO WA NDUGU NDUNGURU WA KU-INVEST NYUMBANI. JOB WELL-DONE JOHN!