ANGALIA LIVE NEWS

Friday, December 10, 2010

UZINDUZI WA TOLEO LA KIPEPEO




•           Mustafa Hassanali kuzindua kipepeo
•           Ni toleo la tatu kwa mwaka 2010, baada ya Perfum d’ amour na Karafuu
•           “Kipepeo” kuzinduliwa Maputo na Luanda kwa pamoja
Mbunifu wa mavazi  maarufu nchini  Tanzania Mustafa Hassanali, atazindua teleo jipya linalojulikana kwa jina la “KIPEPEO” tarehe 10 na 11 ya mwezi wa Disemba 2010, nchini Mozambique na Angola.
Mawazo ya jina la KIPEPEO yametokana na kisiwa cha Marashi ya karafuu Zanzibar kufuatia bustani maarufu na ya kuvutia  ya  Forodhani. Bustani  ambayo ipo katika maeneo ya wazi , pembezoni mwa bahari ya hindi,  eneo ambalo watu wa aina mbalimbali na rika tofauti  hukutana kwa ajili ya chakula cha jioni na kupunga upepo wa Bahari ya Hindi. Bustani ambayo ipo jirani na jemgo maarufu la Ngome Kongwe.

Kutokana na Bustani ya Forodhani  kuvutia kimandhari , watu hufurika hasa wakati wa sikukuu  ya Eid ambapo Wazanzibari  hujumuika pamoja wakiwa na familia zao pamoja na marafiki huku wakiwa wamevaa nguo zenye rangi tofauti tofauti, ambazo zilipelekea kuonekana kama bustani ya Eden kutokana na rangi mbalimbali  za kuvutia zinafanana na mdudu kipepeo.
“Hali hii  ilinivutia sana, ndipo nilipoamua toleo langu la mara hii  kulipa jina la “KIPEPEO”  hii imekuja  kutokana na ukweli kwamba  kipepeo ni mdudu ambae anavutia , hufariji, hutoa matumanini na amekuwa akionekana wazi katika mazingira yoyote kutokana na rangi zake za kuvutia”. Alieleza Mustafa Hassanali
Kipepeo ni neno la kiswahili, ambalo pia  limekuwa na maana nyingine, pamoja na mdudu pia lina maana ya feni ya mokononi ambayo pia inajulikana kama feni ya mswahili, na mara nyingi imekuwa ikitumiwa na wanawake wa mwambao wa bahari. 
Toleo la kipepeo litaiwakilisha Tanzania kimataifa kwa kuoneshwa kwa mara ya  kwanza Luanda nchini Angola Disemba 10 katika onesho la mavazi la kibiashara (The Fashion Business Angola ) na wakati huohuo  litaoneshwa tarehe 11 Disemba  katika onesho la kila mwaka la wiki ya mavazi  Maputo  Mozambique, enesho linalojulikana kama Mozambique Fashion Week, ambalo linafanika kwa mwaka wa sita sasa.
“Natarajia kiiwakilisha Tanzania katika maonesho katika  hayo ya kimataifa na kuzindua toleo la kipepeo kimataifa, katika nchi zinazozungumza lugha ya Kireno na hata nchi nyingine zilizozunguka bahari ya Hindi…. Alimalizia Hassanali.
 Mwaka 2010 Mustafa Hassanali amezindua matoleo matatu, likiwemo la Parfum D’amour alizindua mwezi wa pili huko Douala, Cameroon. Karafuu , Zanzibar mwezi wa Julai na kuoneshwa tena Septemba jinini Arusha   na Octoba Nairobi nchini Kenya. Na sasa ni wakati wa teleo jipya la  Kipepeo litakolooneshwa kwa mara ya kwanza nchini Maputo, Mozambique na Luanda, Angola.

Taarifa Kwa Wahariri.

KUHUSU  MUSTAFA HASSANALI
Mustafa Hassanali, mbunifu wa mavazi na mjasiriamali ambea siku zote amekua akiamini kwamba ‘never say die’ na amekua akitumia kipaji alichonacho katika kubuni mavazi na vitu mbalimbali kwa lengo la kukuza sanaa ya ubunifu kwa sasa na kwa siku zijazo
Kazi  mbalimbali za Mustafa zimekuwa zikikubalika kwa kiwango kikubwa kimataifa. Amesha fanya maonesho  ya kimataifa kwa nchi mbalimbali kama vile  Douala, Cameroon, India International Fashion Week 20009, Naomi Campbell’s Fashion for Relief 2009, Arise Africa Fashion week 2009, Durban & Cape Town Fashion Weeks, Vukani Fashion Awards in Pretoria, Miss Ethiopia Beauty Pageant, Mediterranean Fashion Festival in Sicily, Italy; M’Net Face of Africa, Mozambique, Uganda & Kenya Fashion Weeks.

KUHUSU WIKI YA MAVAZI YA MOZAMBIQUE
Mozambique Fashion Week (MFW), ni tamasha la sanaa na utamaduni na la pekee nchini Msumbiji linalounganisha wabunifu na linalovumbua vipaji mbalimbali ikiwemo ubunifu wa mavazi, pia limelenga kuleta ajira na kufungua njia mpya ya bishara, masoko na mawasiliano kitaalamu katika suala zima la mitindo nchini Msumbiji na kimataifa.

Mozambique Fashion Week ina malengo ya kuimarisha mitindo kitaifa na pia kupanua wigo wa soko la mitindo nchini humo, ikiwemo kuibua vipaji vipya nchini kote.
MFW imeazimia kuleta chachu ya maendeleo ya mitindo na kuwa kivutio kikubwa cha utalii nhini humo, sambamba na kutangaza utamaduni wa nchi ya msumbiji.


KUHUSU FASHION YA KIBIASHARA ANGOLA
Tamasha kubwa kwa ajili ya maonesho ya mavazi na urembo litafanyika nchini Angola Disemba 2010.
Tukio hilo linafanyika kwa mashirikiano kati ya FIL – International Fair of Luanda – na Wizara ya Viwanda na Madini ya nchini humo. Maonesho ya kibiashara ya Angola kwa mwaka 2010 yatawaleta pamoja washiriki zaidi ya 130 wanaojihusisha na masuala ya fashion, mavazi, mapambo ya aina mbalimbali na urembo. Sambamba na maonesho hayo sa kibiashara , zaidi ya wabunifu wa mavazi 20 maarufu kutoka bara la Afrika, Brazil na Portugal watafanya shoo kila siku wakati wote wa Tamasha.  
Fashion Business Angola sio kwa ajili ya shoo peke yake , kwa ujumla ni kuhisiana na kujenga mtandao wa kibiashara kwa wadau wa sanaa ya ubunifu, wazalishaji na wanunuzi, pia kupromoti rasalimali zilizopo barani Afrika kwa waafrika na kimataifa kwa ujumla wake.
###

Saphia Ngalapi
Media & PR Manager
Mustafa Hassanali
PO Box 10684, Dar es Salaam, Tanzania
105 Kilimani Road,   Kinondoni, Dar es Salaam, Tanzania
(opp. Patricia Metzger Health & Beauty Clinic / near French Embassy)
Tel :  +255 (0)22 266 8555
Mobile :  +255 (0)712 099 834
Mail : media@mustafahassanali.net
Web : www.mustafahassanali.net
www.swahilifashionweek.com
www.harusitradefair.com
www.twende.info

No comments: