Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Felchesmi Mramba akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu upungufu wa uzalishaji umeme unaolikabili shirika hilo.Picha na Emmanuel Herman
MATUMAINI ya upatikanaji wa umeme kurejea katika hali ya kawaida yamezidi kufifia kufuatia tamko la Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwamba mgawo huo utaendelea hadi mvua za masika zitakapoanza kunyesha huku lenyewe likipata hasara ya sh 3bilioni kutokana na tatizo hilo.
Tamko la Tanesco limekuja wakati wananchi wakilalamikia mateso na hasara inayotokana na mgawo huo wa umeme ambao sasa unasubiri kudra za Mwenyezi Mungu kuruhusu mvuza za masika kunyesha.
Awali, shirika hilo lilisema mgawo huo ungeisha mwanzoni wa mwezi wa Januari mwaka huu lakini badala yake Taneso siku chache zilizopita ilitangaza kuongeza siku za mgawo kutoka tatu hadi tano kwa wiki.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Felchesmi Mramba, alisema kutokana na kushuka kwa kina cha maji katika bwawa la Mtera, mgawo huo utaendelea.
"Kina cha maji katika bwawa la Mtera kwa sasa kimeshuka mpaka kufikia mita 691.38 juu ya usawa wa bahari, hii ikiwa ni mita 1.38 tu juu ya kina cha chini kinachoweza kuruhusu uzalishaji wa umeme katika bwawa hilo,"alisema Mramba akisisitiza kwamba makali ya mgawo yataendelea kwa kuwa uzalishaji umeme katika bwawa hilo sasa si wa kuaminika.
Mramba aliongeza kwamba, mwaka jana kina cha maji kilikuwa mita 696.40 juu ya usawa wa bahari hivyo kwa sasa mahitaji ya umeme yameongezeka kwa wastani wa asilimia 10 au megawati 80 mpaka 100 kila mwaka.
Alifafanua kwamba, mitambo yote ya kuzalisha umeme katika gridi ya taifa ina uwezo wa megawati 1,006, mitambo ya maji ikiwa na uwezo wa megawati 561 huku mitambo ya gesi na mafuta ikiwa na uwezo wa kuzalisha megawati 445. Kutokana na uhaba wa maji, alisema hivi sasa mitambo ya maji inazalisha wastani wa megawati 180 tu, wakati mitambo ya mafuta na gesi ikizalisha wastani wa megawati 290.
"Hii inafanya jumla ya umeme wote unaopatikana kwenye gridi ya taifa kuwa wastani wa megawati 470 ambayo ni asilimia 67 tu ya mahitaji ya wastani ya umeme au asilimia 57 tu ya mahitaji ya juu katika gridi ya taifa,"alisema. Kaimu mkuu huyo wa Tanesco aliongeza kwamba, mpaka sasa kuna upungufu wa wastani wa megawati 230 katika gridi ya taifa .
Kwa mujibu wa Mramba, upungufu huo wa maji katika mabwawa ya Mtera,Nyumba ya Mungu, Kidatu, Kihansi na Pangani ndiyo chanzo kikubwa cha mgao wa umeme unaoendelea nchini.
"Upungufu huu mkubwa wa maji katika mabwawa yetu umetokana na ukweli kwamba, hakukuwa na mvua za kutosha za vuli mwaka jana katika maeneo mengi ya nchi yetu na pia mvua za masika ambayo huanza mapema katika mikoa ya kanda ya kati na kusini magharibi zimechelewa kuanza,"alisema Mramba Mramba aliongeza kuwa, tatizo hilo la umeme litakuwa limefikia kikomo pindi itakapofikia mwaka 2013 mara baada ya miradi ya kuzalisha umeme nchini kukamilika.
Akirejea kile kinachoonekana ni ‘wimbo’ wa ahadi za miradi hiyo ‘hewa’ , aliitaja tena kwamba ni pamoja na mradi wa Mnazi bay, ambao utazalisha umeme wa megawati 300, Kinyerezi megawati 240, Somanga Fungu megawati 230, Kiwira-megawati 200 na mradi wa Singida wa kuzalisha umeme wa upepo megawati 100. Alisema miradi yote hiyo inatarajiwa kukamilika ifikapo mwaka 2013 na kumalizika kwa tatizo hili la mgawo wa umeme nchini.
Katika hatua nyingine, Mramba alisema ujumla tatizo hilo la mgao wa umeme lililopo kwa sasa ni la muda na linatarajiwa kwisha au kupungua sana kutokana na jitihada mbalimbali zinazoendelea kufanywa.
Akielezea jitihada zinazifanywa na serikali alisema ni pamoja na kununua mafuta ya kuendesha mtambo wa IPTL ili kuzalisha megawati 80 kwa siku. Katika kufafanua hilo, alisema mafuta hayo tayari yameshanunuliwa na tayari yameshawasili IPTL na hiyo itaweza kupunguza mgao wa umeme kwa megawati 70.
Alisema shirika linawasiliana na serikali kuangalia uwezekano wa kupata mitambo ya dharura ili kukabiliana na hali inayoweza kujitokeza endapo mvua za masika zitakuwa chini ya wastani.
"Tunajua wananchi wanatuchukia sana kwa sasa hivi lakini hata sisi tunasikitika kwa mgao huu unaoendelea na tunajua unaleta hasara kwa taifa,''alisema. Pia kwa mujibu wa Mramba, kutokana na mgawo huo shirika la umeme mpaka limeshapata hasara ya shilingi bilioni 3.

CHANZO:MWANANCHI
No comments:
Post a Comment