Advertisements

Wednesday, March 30, 2011

HARUSI TRADE FAIR 2011

The wedding Fair Organizer, Mustafa Hassanali (right) speaks during Press Conference today at his Office


  • Monyesho ya Harusi yawa ya kitaifa
  • Mavazi ya Harusi kuonyeshwa tarehe 2 April
  • Mdahalo wa kwanza wa Harusi kuzinduliwa katika maonyesho.

Maonyesho ya mavazi ya kwanza na ya kipekee yanatarajiwa kuanza kurindima mwanzoni mwa mwezi ujao kuanzia tarehe 1 mpaka 3 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam, huku maandalizi ya maonyesho hayo kwa mwaka huu yakiwa yamekamilika yakiwa na washiriki zaidi ya 51 waliothibitisha kushiriki.


“mwaka huu tuna washiriki mbalimbali na toka sehemu tofauti wakiwemo kutoka Arusha na Zanzibar, hii ni kuthibitisha tu kwamba maonyesho haya sasa ni ya kitaifa zaidi na si Dar es salaam tu” alisema Mustafa Hassanali, muaandaaji wa maonyesho hayo.

Kama ilivyokuwa kwa maonyesho ya mwaka jana , siku ya pili kwa mwaka huu itakuwa ni kwa wabunifu mbalimbali na wauzaji wa magauni ya Harusi kuonyesha mavazi yao katika Maonyesho ya nguo za Harusi, ambapo hii itaanza saa mbili usiku. Kwa kweli hii si ya kukosa kwa wale wanaotarajia kufunga ndoa.
“mwaka huu tumeongeza kipengele kipya cha Mdahalo wa Harusi ambapo wataalamu na waliobobea katika mambo mbalimbali ya Harusi watatoa mada, hii ni pamoja na kuzungumzia yanayopasa katika Harusi, urembo, jinsi ya kuchagua mavazi ya Harusi, keki, mapambo, bila kusahau yahusuyo wanaume katika Harusi. Hii ni pamoja na kuwaleta pamoja wahusika wa Harusi, wataalamu, na kupata habari toka kwa wenye utaalam wa masuala hayo hapa nchini.” Aliongezea kusema Hassanali.

“kwa siku tatu za maonyesho ya Harusi kwa mwaka huu, milango itakuwa wazi kuanzia saa 4 asubuhi kila siku mpaka saa 2 usiku, na tunawaomba sana wadau na watarajiwa wa Harusi kutembelea maonyesho ya mwaka huu, na kuonyesha ushirikiano kwa wajasiriamali wetu nchini.” Alimalizia kusema Mustafa Hassanali.
Baadhi ya washiriki wa maonyesho wa mwaka huu ni: Some of the exhibitors for Harusi Trade Fair 2011 are: Lotus Creative Concepts, Nadd House Events Hire,  Zanzibar Weddings, Fannina Investments, Endepha Events Planners,Luxe Papers, Paper Designs, Vayle Springs, Upper Zonal Trading, River Blues Tanzania Ltd, MH Gallery,Kinara Mobile Studio, Dar City, Slice of Wedding,Markham Executive Suites,The Flying Chefs, Mustafa Hassanali Wedding, Malaika Event Designs & Rentals, GRM Production, Bluecheriemoe, DIA’s, Metro Fashion, Rose Fashion Designer, TANZANIA HAIR INDUSTRY, NORBROS Collection, Manju Msitta, Caros Cakes& Hot Brades, Moevenpick Royal Palm Hotel, Sheer Illusion and Daily News.


Maonyesho ya Harusi kwa mwaka huu yamedhaminiwa na Clouds FM, Daily News, Habari Leo, Global Outdoor Systems, Image Masters, Ultimate Security, Vayle Springs, Eventlites na 361 degrees.

Kwa Mhariri.

Maonyesho ya Harusi, yatafanyika kwenye ukanda wa pwani wa Afrika Mashariki, Dar es salaam Tanzania.

Harusi ni neon la Kiswahili linalosomama katika maana ya kuwaleta pamoja wawili wa jinsia mbili tofauti katika maisha ya pamoja kama mke na mume.  Ni wazo la mbunifu wa mavazi Mustafa Hassanali katika mwaka wa 2009 kuwa na maonyesho makubwa kama haya ya Harusi.

Ni maonyesho yanayofanyika mara moja kwa mwaka huku yakiwafikia takriban watu 10,000 wanaotarajia kufunga ndoa, familia na marafiki zao, ambao kwa namna moja au nyingine wanahusika katika maandalizi ya Harusi, huku maonyesho haya yakiwaleta pamoja wahusika na wataalamu wa mambo ya Harusi katika soko moja la siku tatu


Kwa maelezo zaidi tembelea www.harusitradefair.com




Mfaume Shaban
Media & PR Manager
Mustafa Hassanali
PO Box 10684, Dar es Salaam, Tanzania
105 Kilimani Road,   Kinondoni, Dar es Salaam, Tanzania
(opp. Patricia Metzger Health & Beauty Clinic / near French Embassy)
Tel :  +255 (0)22 266 8555
Mobile :  +255 (0)655 501 526
Mail : media@mustafahassanali.net
Web : www.mustafahassanali.net
www.swahilifashionweek.com
www.harusitradefair.com
www.twende.info

No comments: