Smart Meter ni mita mpya ya umeme yenye uwezo wa kurekodi matumizi yako ya umeme ya na kutuma matumizi yako kwenye kampuni ya umeme kwa ajili ya kujulisha kampuni yako ya umeme matumizi yako ya kila siku na kitu gani unachotumia ndani ya nyumba yako kinachokula umeme zaidi pia inasaidia kampuni ya umeme kusoma matumizi yako ya umeme bila kutuma msomaji mita nyumbani kwako.
Mita hizi zlianzia California na Texas na sasa zinafungwa Washington,DC kwa hiyo watu wa Maryland na Virginia mkae mkao wa kula zitaingia huko muda si mrefu kwenye miji yenu.
Huko California ilibidi polisi kuingilia kati ilikusaidia kufungwa kwa mita hizo kwani wakazi wa California walifanya maandamano ya kuzuia kufungwa kwa mita hizo kwa kisingizio kwamba zinapandisha bili ya umeme na nyumba moja ilibidi itolewe kwa kusababisha alarm ya nyumba kulia mfululizo.
No comments:
Post a Comment