Advertisements

Tuesday, March 29, 2011

UBALOZI WA TANZANIA WASHINGTON DC WAITANGAZA TANZANIA MASHULENI MARYLAND

Ubalozi wa Tanzania Washington DC kwa kushirikiana na kampuni ya Utalii ya Vacation 2 Africa inayomilikiwa na Mtanzania Thomas Andrerico Kisura imeanza na utaratibu mpya wa kuitangaza Tanzania kiutalii kwa wanafunzi wa shule mbali mbali hapa Marekani. Mwishoni mwa wiki Bw. Thomas Andrerico Kisura ambae amekuwa mshirika wa karibu wa Ubalozi katika kuitangaza Tanzania na vivutio vyake vya Utalii alishiriki katika maonyesho maalum yaliyokuwa na mvuto wa aina yake ambapo wanafunzi zaidi ya 500 walishiriki. Tanzania ilitangazwa vizuri na kufahamika vyema na Ubalozi unamshukuru Bw. Thomas Anderico Kisura kwa juhudi zake na uzalendo wake wa kushirikiana na Ubalozi kuitangaza nchi yetu.
Picha juu na chini ni Bw. Thomas  Andrerico Kisura akiwa katika zoezi kuitangaza Tanzania kwa wanafunzi wa Garriison Elementary huko Baltimore Maryland.
Seif Msabaha nae akiwa katika zoezi la kumsaidia Thomas Kisura kuitangaza Tanzania
Seif Masabaha (shoto) akisikiliza utambulisho wa Thomas Kisura kwa wanafunzi na Principal wa Garriison Elementary huko Baltimore Maryland
Kushoto ni Ada Brown mwandaaji wa onesho hili katika picha ya pamoja na Thomas Kisura(kati) na Chief wa Gabon kama alivyokua akijiita ambae alikua anawakilisha Ubalozi wao kwenye maonyesho hayo.

No comments: