Advertisements

Thursday, April 28, 2011

Malawi na Uingereza 'zatunishiana misuli'-BBC

Uingereza imetoa amri kwa balozi wa Malawi kuondoka nchini humo kufuatia kufukuzwa "kusiko sawa" kwa balozi wa Uingereza nchini Malawi.
Bingu
Rais Mutharika
Balozi wa Uingereza Fergus Cochrane-Dyet alitakiwa kuondoka Malawi baada wa kukaririwa katika waraka uliovuja akisema rais havumilii kukosolewa.

Mjumbe mmoja wa UIngereza ameonya kuwepo kwa "madhara makubwa", kwa mujibu wa waraka wa siri ambao BBC imeuona.
Asilimia 40 ya bajeti ya serikali ya Malawi inatoka nchi za nje. Uingereza ndio mhisani mkubwa zaidi.
Mualiko wa serikali ya Malawi katika haruzi ya Kifalme umefutwa pia.
Kwa mujibu wa waraka wa kibalozi uliochapishwa katika gazeti moja wiki iliyopita, Bw Cochrane-Dyet alimuelezea rais wa Malawi Bingu wa Mutharika kuwa anazidi kuwa "dikteta na kutovumilia kukosolewa".
Alisema wanaharakati wa vyama vya kiraia wamekuwa waoga baada ya kupata simu za vitisho na kusema serikali ilikuwa inazuia uhuru wa vyombo vya habari na watu wa makabila madogo.
Mwaka jana, kutokana na shinikizo kutoka kwa nchi wahisani, aliwapa msamaha wapenzi wawili wa jinsia moja waliofungwa gerezani kutokana na uhusiano wao wa kimapenzi, jambao ambalo ni kosa nchini Malawi.

No comments: