NDUGU WANA NEW YORK METRO,
Jina langu naitwa Hajji Khamis,mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio maeneo ya New York,New Jersey,Pennsylvania na Connecticut.
Kwa kuanza nnawaomba wana New York metro wenzangu tujitokeze kwa wingi ili tuweze kuchagua viongozi watakaotuwakilisha katika kipindi hiki.Pia ningependa kuwashawishi wale wote ambao hawakujisajili na jumuiya yetu wafanye hivyo kupitia kwa wahusika na wale ambao hawatopata nafasi waje kwenye uwanja wa uchaguzi wataruhusiwa kujisajili hapo na wataweza kupiga kura na kuchagua viongozi wao.Anuani ya mahali tafadhali ingia kwenye website ya jumuiya(www. nytanzaniancommunity.org). Tafadhali tufike saa nane kamili bila kuchelewa.
KAMA MGOMBEA WA NAFASI YA MWENYEKITI WA MWANZO WA JUMUIYA YETU,
1) Lengo langu kuu ni kuwaunganisha wana New York Metro bila kujali dini,kabila ama jinsia.Kuleta mapenzi baina yetu na kujenga moyo wa kuaminiana.
2) Kubuni programu zitakazotuwezesha kuwapatia watoto wetu scholarship ili waweze kuleta ushindani mashuleni.Watoto wetu ndio future yetu.
3) Kubuni njia zitakazosaidia wanacommunity kuingia kwenye ulimwengu wa ujasiriamali na kadhalika.
Wana New York kwenda mbele tunahitaji umoja na kuwa na umoja imara tunahitaji viongozi imara wenye moyo wa kujitolea kusaidia wanacommunity.Historia yangu inaonyesha ushiriki wangu na uwezo wangu kusikiliza,kuwasiliana na kuwaunganisha wanajumuiya.
Jumuiya yetu hii ni muendelezo wa jumuiya tuliyoianzisha mwaka jana chini ya uongozi wangu wa muda.Katika kuhakikisha tunamshirikisha kila Mtanzania anaeishi maeneo haya ya Metro,tuliunda kamati iliyohakiki jumuiya ile na kwa kuafikiana tumeafiki wakati muafaka wa kuchagua viongozi wa jumuiya yetu.
Uongozi wangu wa muda uliweza kuendeleza mahusiano mazuri na balozi zetu mbili za Washington na New York yaliyopelekea kufanikisha mengi ukiwemo ujio wa Muheshimiwa Waziri Mkuu.Uongozi wangu ulimvutia waziri mkuu kiasi cha kuamua kutufanyia fund raise ya zaidi ya dola $10,000.00.Pia tulishirikiana kwa karibu katika misiba na mengineyo.
Wana New York Metro,naomba kura zenu ili niweze kumalizia kile nilichokianza kwa manufaa ya wote.Tujumuike pamoja ili tujenge jumuiya iliyo imara.Tujumuike kuwaleta wana New York Pamoja.
UMOJA NI NGUVU
MGOMBEA UENYEKITI
HAJJI KHAMIS.
Jina langu naitwa Hajji Khamis,mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio maeneo ya New York,New Jersey,Pennsylvania na Connecticut.
Kwa kuanza nnawaomba wana New York metro wenzangu tujitokeze kwa wingi ili tuweze kuchagua viongozi watakaotuwakilisha katika kipindi hiki.Pia ningependa kuwashawishi wale wote ambao hawakujisajili na jumuiya yetu wafanye hivyo kupitia kwa wahusika na wale ambao hawatopata nafasi waje kwenye uwanja wa uchaguzi wataruhusiwa kujisajili hapo na wataweza kupiga kura na kuchagua viongozi wao.Anuani ya mahali tafadhali ingia kwenye website ya jumuiya(www.
KAMA MGOMBEA WA NAFASI YA MWENYEKITI WA MWANZO WA JUMUIYA YETU,
1) Lengo langu kuu ni kuwaunganisha wana New York Metro bila kujali dini,kabila ama jinsia.Kuleta mapenzi baina yetu na kujenga moyo wa kuaminiana.
2) Kubuni programu zitakazotuwezesha kuwapatia watoto wetu scholarship ili waweze kuleta ushindani mashuleni.Watoto wetu ndio future yetu.
3) Kubuni njia zitakazosaidia wanacommunity kuingia kwenye ulimwengu wa ujasiriamali na kadhalika.
Wana New York kwenda mbele tunahitaji umoja na kuwa na umoja imara tunahitaji viongozi imara wenye moyo wa kujitolea kusaidia wanacommunity.Historia yangu inaonyesha ushiriki wangu na uwezo wangu kusikiliza,kuwasiliana na kuwaunganisha wanajumuiya.
Jumuiya yetu hii ni muendelezo wa jumuiya tuliyoianzisha mwaka jana chini ya uongozi wangu wa muda.Katika kuhakikisha tunamshirikisha kila Mtanzania anaeishi maeneo haya ya Metro,tuliunda kamati iliyohakiki jumuiya ile na kwa kuafikiana tumeafiki wakati muafaka wa kuchagua viongozi wa jumuiya yetu.
Uongozi wangu wa muda uliweza kuendeleza mahusiano mazuri na balozi zetu mbili za Washington na New York yaliyopelekea kufanikisha mengi ukiwemo ujio wa Muheshimiwa Waziri Mkuu.Uongozi wangu ulimvutia waziri mkuu kiasi cha kuamua kutufanyia fund raise ya zaidi ya dola $10,000.00.Pia tulishirikiana kwa karibu katika misiba na mengineyo.
Wana New York Metro,naomba kura zenu ili niweze kumalizia kile nilichokianza kwa manufaa ya wote.Tujumuike pamoja ili tujenge jumuiya iliyo imara.Tujumuike kuwaleta wana New York Pamoja.
UMOJA NI NGUVU
MGOMBEA UENYEKITI
HAJJI KHAMIS.
No comments:
Post a Comment