ANGALIA LIVE NEWS

Monday, May 16, 2011

Ghasia zaongezeka kwenye mipaka ya Israel-VOA

Polisi wa Israel wakimtia nguvuni mmoja wa waandamanaji wa kipalestina.
Polisi wa Israel wakimtia nguvuni mmoja wa waandamanaji wa kipalestina
Mashahidi na maafisa wa Lebanon wanasema majeshi ya Israel yaliuwa watu wapatao watano na kujeruhi zaidi ya hamsini.
Maandamano kadhaa katika mipaka ya israel  ya kuunga mkono Wapalestina yaligeuka ghasia mbaya  na kupelekea watu 10 kufariki dunia na mamia wengine kujeruhiwa.
Mashahidi na maafisa wa Lebanon wanasema majeshi ya Israel yaliuwa watu wapatao watano na kujeruhi zaidi ya hamsini wakati walipowafyatulia risasi waandamanaji ili kuwazuia kuvuka na kuingia Israel kutoka Lebanon.
Waandamanaji huko Syria pia walijaribu kuvunja uzio wa mpaka katika eneo linalokaliwa  na Israel la milima ya  Golan. Afisa mmoja wa Syria na mashahidi wamesema majeshi ya Israel yalifyatua risasi, kuuwa wanne na kujeruhi watu wapatao 45.

No comments: