Mahakama ya Mkoa wa Shinyanga imemwachia kwa dhamana Mbunge wa Meatu, Meshack Oporukwa (Chadema), baada ya kushikiliwa kwa saa 24.
Akizungumza na NIPASHE jana kwa njia ya simu kutoa mkoani humo, Oporukwa alisema aliachiwa kwa dhamana jana saa 8:30 alasiri baada ya kutimiza masharti ya dhamana.
Oporukwa alisema alisomewa mashitaka mawili ambayo ni ya kuitisha mkusanyiko usio halali na shitaka la pili ni kukaidi amri ya Kamanda wa Polisi wa Wilaya (OCD) wa kuitisha mkutano usio halali.
Oporukwa alisema mahakama ilimtaka awe na wadhamini wawili na mali zisizohamishika zenye thamanai ya Sh. 500,000 kila mmoja.
Alisema alidhaminiwa na mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Rachel Mashishanga na Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Shinyanga, Yasine Swedi.
Kesi hiyo ilihairishwa hadi June 2, mwaka huu.
Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga lilimkamata mbunge huyo baada ya kufanya mkutano wa hadhara katika kijiji cha Nkoma, wilayani Meatu alipokuwa anawashukuru wananchi kwa kumpigia kura na Jeshi la Polisi lilidai kuwa alivunja sheria kwa kufanya mkutano wa hadhara na kuzidisha muda.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment