TIMU ya soka ya Taifa, Taifa Stars imeshindwa kutamba mbele ya Afrika Kusini ‘Bafana Bafana’ baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Wageni walipata bao katika dakika ya 43 mfungaji akiwa Siyabonga Sangweni aliyefunga bao hilo kwa kichwa kutokana na mpira wa kona ambao uzembe wa kipa wa Stars, Juma Kaseja na beki yake, ulifanya washindwe kuokoa.
Katika kipindi cha kwanza cha mechi hiyo, Taifa Stars walipata nafasi lakini wachezaji wake John Bocco ambaye hakuonesha cheche zozote, Julius Mrope na Mohamed Banka walikuwa wakipoteza nafasi walizopata.
Kipindi hicho, Stars walionekana kucheza vizuri sehemu ya kiungo lakini mbele washambuliaji wake walikosa mbinu za umaliziaji.
Kipindi cha pili kocha wa Stars Jan Poulsen alifanya mabadiliko kwa kumtoa Kesi Chombo na kumuingiza Mwinyi Kazimoto katika dakika ya 47, mabadiliko ambayo yalizidisha matumaini kwa Stars kwani walizidi kuimarika.
Stars nusura iandike bao katika dakika ya 60 lakini mshambuliaji wake Bocco alishindwa kuiwahi krosi ya Shadrack Nsajigwa akiwa kwenye nafasi nzuri ya kufanya hivyo, dakika chache baadae kocha wa Stars akafanya mabadiliko langoni ambapo alimtoa Kaseja na nafasi yake kuchukuliwa na Shaaban Dihile.
Stars ilikosa bao lingine katika dakika ya 78 pale Nsajigwa alipokuwa ndani ya 18 na kuachia shuti kali lakini likatoka nje.
Katika mechi hiyo wachezaji Mrope, Kazimoto, Salum Machaku walichangamsha timu hasa katika dakika 15 za mwisho ambapo walishambulia sana na kufanya Bafana Bafana ‘wapoteane’.

CHANZO:HABARI LEO
------------------------------------------------------
VIJIMAMBO inaomba radhi kwa wadau wote kwa ile habari ya Stars kusawazisha bao,kulikua na makosa ya mawasiliano na Ripota wa Vijimambo Bongo,kumradhi kwa usumbufu wote uliotokea
No comments:
Post a Comment