NI dunia na mambo ya kisasa. Chapuo la mabadiliko linazidi kupata meno makali. Zamani ilionekana mwanamke akitongoza ni haramu lakini sasa mambo ni bambamu. Mtu yake kauli, moyo ukivutika, haraka sana anatua mzigo kwa mhusika.
Vipi ubaki na jakamoyo wakati anayekufanya moyo wako ufukute yupo karibu? Hii ni mada ambayo nilianza nayo wiki iliyopita, mastaa wakubwa Bongo, Stara Thomas, Sakina Lyoka, Tayana Tibenda, Sauda Mwilima na Latifa Idabu ‘Badra’ walieleza mitazamo yao.
Vipi ubaki na jakamoyo wakati anayekufanya moyo wako ufukute yupo karibu? Hii ni mada ambayo nilianza nayo wiki iliyopita, mastaa wakubwa Bongo, Stara Thomas, Sakina Lyoka, Tayana Tibenda, Sauda Mwilima na Latifa Idabu ‘Badra’ walieleza mitazamo yao.
Natoa nafasi ya mastaa nao kutoa maoni ili kuchanganya mawazo. Nikiamini kwamba mwisho unaweza kupata kikubwa zaidi. Kabla sijafafanua kuhusu kile nilichonacho, naomba nitoe nafasi kwa warembo wengine maarufu Bongo ambao wanajieleza ifuatavyo;
KHADIJA SHAIBU ‘DIDA WA G’
Anasema kuwa mwanaume na mwanamke wote wana matamanio sawa, kwa hiyo hakuna ubaya wowote kwa mtoto wa kike kueleza kilichomo ndani ya nafsi yake endapo nafasi ya kufanya hivyo anayo.
“Inafaa kuzungumza ukweli na wala mwanamke kumtamkia mwanaume kuwa anampenda siyo uhuni. Mimi naamini kila mmoja anatakiwa kuwa huru kueleza hisia zake,” Dida.
LULU MATHIAS SEMAGONGO ‘AUNTY LULU’
“Mwanamke kumtongoza mwanaume siyo sawa. Kwanza ni kwenda kinyume na mila zetu. Kama mwanamke anakuwa wa kwanza kupenda, basi anachopaswa kufanya ni kuonesha dalili kwa huyo mwanaume aliyempenda.
“Mimi nikimtaka mwanaume, namtoa out kama vile kwenda kupata naye chakula, nitampa zawadi mbalimbali. Hiyo ni njia ambayo ukiifanya, husaidia kuhamisha upendo kutoka kwa mwanamke kwenda kwa mwanaume ambaye mwisho hutamka,” Aunty Lulu.
ANNETTE JOHN
Huyu ni Miss East Africa namba mbili mwaka 2009 pia Miss Ilala namba tatu 2008. Anasema: “Mwanamke ana hisia kama mwanaume na kila mmoja ana uhuru wa kupenda.
“Mimi nashauri wanaume wawe wanaheshimu hisia za wanawake. Mwanaume akiambiwa anapendwa na mwanamke asimdharau. Kama ilivyo kwa mwanaume alivyo huru kukubaliwa au kukataliwa anapomtongoza mwanamke, na kwa mwanamke pia inawezekana.”
DOREEN PONERA ‘PIPI’
Mwanamuziki wa Bongo Fleva. Anasema kuwa hivi sasa anahisi asilimia kubwa ya wanawake ndiyo wanaowatongoza wanaume.
“Siyo uhuni kabisa. Mwanamke anaweza kueleza hisia zake za kupenda, akaweka malengo kwa mwanaume aliyempenda. Mwanamke ana hisia za kweli, kwa hiyo siyo umalaya mwanamke kusema ukweli wa moyo wake,” Pipi.
RUTH SUKA ‘MAINDA’
Staa huyo amesema kuwa hata kwenye vitabu vya Mungu hakuna sehemu inayoonesha kuwa mwanamke anaweza kumtongoza mwanaume.
“Hata kama ni maendeleo lakini ukweli ubaki kuwa mwanaume ndiye anayetakiwa kumtakia mwanamke. Huu ndiyo utamaduni wetu na hata vitabu vinaeleza hivyo,” Amanda.
UNASHIKA LIPI?
Kwa jumla, mastaa 10 wamezungumza kuanzia toleo lililopita. Watatu ndiyo wamesema mwanamke hatakiwi kutongoza, saba wameeleza kwamba inawezekana na siyo uhuni.
Katika hao saba, wawili wamesema wao hawawezi kutongoza. Kwa mahesababu hayo, ni asilimia 50 kwa 50 lakini shika kile ambacho unaona kina hekima ndani yake kwenye yaliyoelezwa na mastaa hao.
SIYO UMALAYA
Asilimia kubwa ya wanawake ambao huwatongoza wanaume wana mapenzi ya kweli. Idadi ya wanaume matapeli ni kubwa, wanaweza kusema wanapenda kumbe ndani ya nafsi zao kuna kitu kingine kabisa.
Kimaumbile na kisaikolojia, mwanamke anapofikia hatua ya kumwambia mwanaume kuwa anampenda, anakuwa amefikia kikomo cha kuvumilia. Mwanaume anayeambiwa hayo maneno, ayasikilize kwa makini na ayaheshimu. Akimdharau kwamba ni malaya, atakuwa amepoteza madini yenye thamani kubwa.
Pamoja na maneno hayo, tutambue uhalisia wa maumbile yetu na tujue desturi zetu zipoje.
Eid El El-Mubarak.
www.globalpublishers.info
No comments:
Post a Comment