Kwanza kabisa nampongeza Mama Balozi Maajar kutuletea sherehe za uhuru hapa DMV. Imepita miaka kadhaa bila ya sisi Watanzania tunaoishi hapa DMV bila kuwa ya sherehe zetu za kitaifa.
Pia nawapongeza wanakamati wa DICOTA waliojitolea kufanyika zoezi hili la sherehe hizi ili ziweze kufanikiwa. Inaeleweka wazi Tanzania kama Taifa tumepitia kwenye nyanja mbali mbali. Mimi binafsi sikutegemea kuwapo kwa sherehe za miaka 50 ya Uhuru wetu.
Nikiwa kama Mtanzania hakuna kitu ninochojivunia kama Uhuru. Nimesikiliza mahojiano ya vijimambo na Mama Balozi ,yamenigusa sana kuona kwamba hatimaye Tanzania tumepata mwakilishi mwenye mwelekeo sahihi kwa sisi Watanzania .
Wapo vijana wengi wa Kitanzania ambao wamesoma na ni hazina kubwa Taifa letu , kwa ujumla kila Mtanzania aliyeopo hapa USA ni hazina kwa taifa letu. Kwa muda mrefu nimekuwa nikijiuliza kama sisi watanzania tunaoshi nje tunawezaje kuchangia maendeleo ya Taifa letu , yapo mambo mengi ambayo tunaweza kuyafanya kwenye ngazi ya familia na ukoo yote hayo yakawa ni sehemu Gross Domestic Product (GDP) ya taifa letu.
Yapo mambo mengi ya msingi Mama Balozi Majaar ameyagusia kwenye mahojiano yake yamenifurahisha na kunitimia moyo. Ombi langu kwa Watanzania wa DMV tujitokeze kwa wingi ili kufanikisha sherehe zetu za Uhuru.
Uhuru huu ni wetu, Watanzania tuwaenzi wale waliojitolea mhanga kutuletea Uhuru . Tujitokeze ili tumpe nguvu Mama Balozi awe anatuletea vitu kama hapa DMV; tukumbuke wapo watanzania wa majimbo mbalimbali wangependa sherehe hizi zifanyike kwenye maeneo yao. Hizi si sherehe za CCM , CHADEMA wala CUF ni zetu Watanzania wote Bara na Visiwani bila kujali itikadi zetu za kisiasa.
Wapo wanaohoji kiingilio cha dola 90, kwa maelezo ya Mama Balozi ukiangilia manufaa ya mkutano mzima sioni sababu ya kuhoji; majibu ya maswali yetu yapo kwenye mahojiano ya Mama Balozi. Wana DMV tuwe kitu kimoja na tujivunie utaifa wetu.
Ahsante Vijimambo.
Msikilize Tena Mh.Balozi Maajar
6 comments:
unafikiri .utapewa ubosi na wewe nao.
NICE ONE, FULL KUPANGILIA ..JAMANI I MISS HER,MH BALOZI MAAJAR..GOD BLESS HER ALWAYS.
Mtanzania amefariki mpaka sasa hela ya akumsafirisha haijafika. Ubalozi ulitakiwa uwe mstari wa mbele kusaidia mwili wa Marehemu uende nyumbani, ikiwa ni kuhamamsisha michango. badala yake mnasisitaza DICOTA. Marehemu anajihitaki akapumzike.
Mimi ni bosi ndani ya nafsi yangu, sihitaji mtu anipe ubosi, tujitahidi kubadilika hizi nadharia za mrengo wa kushoto ndizo zinazotuletea mipasuko ndani ya jamii yetu hapa DMV. Athari za migawanyiko ndani ya jamii yetu ndiyo tatizo, wapo watu wanaoleta mitafaruku binafsi ndani ya jamii. Cha msingi watanzania tukae chini turudishe umoja wetu hilo ndilo suluhisho pekee. Miaka tulikuwa tunapata mchango kwa siku 2 tu hata sasa hivi hatushindwi. Ubalozi una majukumu yake wengi hatukuletwa na serikali. Jiulizeni wale waliokuwa mstari wa mbele kuleta migongano ndani ya jumuiya wapo wapi? Sisi kama vijana ni lazima tushikamane hakuna haja ya kuanza kuulaumu ubalozi wakati mwingine tujunge mazoea ya kukubali lawama.
Hiyo imekaa poa kabisa,hata kule nyumbani serikali haituchangii kwenye misiba na wala haijatuleta hapa sisi ni ndugu jamani,tumsafirishe mwenzetu
"Ubalozi una majukumu yake...." including cater for welfare of people in that foreign country !! anyway sitaki kuongelea hilo zaidi!
ni kweli kwamba umoja ni kitu muhimu!
nilitaka kuuliza kuhusu dicota mchango tunaotakiwa kuchangia ni kwa ajili ya siku zote 3 , au, na itakua kukutana ni saa ngapi hadi saangapi?pia kutakua na usafiri mf. kutoka DC hadi huko, I mean hata wa kulipia?
thank u 4 u r gud job Luke, keep doing it right !!
Post a Comment