MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imeitoza faini ya sh. milioni 100 CHADEMA, baada ya kubainika inakwepa kodi tangu ilipoanzishwa mwaka 1992. TRA pia imeanza kukata kodi mshahara wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa na watumishi wengine wa CHADEMA. Habari za kuaminika kutoka ndani TRA zilisema ulipaji faini unaanza mara moja, baada ya uchunguzi kukamilika na kuonyesha chama hicho hakilipi kodi.
“Tumemaliza uchunguzi na kubaini CHADEMA hailipi kodi ya mishahara ya kila mwezi ya watumishi wake tangu ilipoanzishwa,’’ kilisema chanzo chetu cha habari.
Imeelezwa kuwa, CHADEMA imekiuka sheria na kanuni za ulipaji kodi, zinazotaka mtu, kampuni au taasisi yoyote kulipa kodi TRA.
“Ijapokuwa tangu ilipoanzishwa ilikuwa hailipi kodi, katika uchunguzi tulipata taarifa za kuanzia mwaka 2000 hadi sasa zinazoonyesha hailipi kodi,’’ kilisema chanzo hicho.
Kutokana na hilo, chama hicho kinapaswa kulipa faini ya sh. milioni 100 na kimeamriwa kulipa kodi ya mishahara ya watumishi wake kuanzia mwezi uliopita.
Chanzo hicho kilisema CHADEMA imeiandika barua TRA ikidai wanacholipana ni posho na si mishahara.
Hata hivyo, sheria ya kodi inaeleza kiwango chochote cha posho kinachozidi kima cha chini cha mshahara kinapaswa kukatwa kodi.
Watendaji ambao TRA imeanza kuwakata kodi ni Dk. Slaa, ambaye analipwa mshahara wa zaidi ya milioni 7.4, fedha ambazo ni nyingi kuliko mshahara wa mbunge.
Mshahara huo unatokana na mapendekezo ya Azimio la Kamati Kuu ya chama hicho iliyokutana Januari 29 na 30, mwaka huu, mjini Dar es Salaam, ambapo mshahara huo umegawanya katika sehemu sita.
Sehemu hizo ni posho ya mwezi, fedha za mafuta, majukumu, viburudisho, nyumba na utendaji kazi, ambapo mshahara wa mwezi ni sh. 2,300,000.
Fedha za mafuta ni sh. sh. 1,387,000 kwa wastani wa lita 750 kwa mwezi, huku fedha za majukumu zikiwa sh. 575,000, mawasiliano sh. 460,000 na nyumba sh. milioni moja.
Posho kwa ajili ya viburudisho sh. 462,500 na utendaji kazi sh. 989,000. Mshahara huo umefanywa maalumu kwa Dk. Slaa pekee na iwapo chama hicho kitapata katibu mkuu mwingine hawezi kulipwa mshahara kama huo.
UHURU
3 comments:
GAZETI LENYEWE UHURU (CCM) ? HAWANA JIPYA.
I feel CCM in this foolish.Tena wameweka milioni 100 ili kutoa the exact amount ya mchango Chadema walosaidiwa na Sandoro.Hivi kweli hamna mwenye akili mmoja kati yao wenyewe (CCM) wa kuwaambia CCM waache michezo ya kitoto.Tactics za za kijinga sana,kupelekana jela ili wawapotezee muda that's so last year.
Basi hata kutekeleza sheria zetu kodi imekuwa ni CCM? Nilitegemea mwanasiasa mkongwe kama Dr. Slaa yeye mmwenyewe aipeleke kodi yake hata kama TRA walizembea kutekeleza majukumu yao, huo ndio uzalendo. Hatujatinga ikulu hatutaki kulipa kodi,je tukiingia mjengoni itakuwaje?
Post a Comment